Sunday, September 22, 2013

Maajabu:Nyani Wenye Njaa Wawavizia Wanawake Wakitoka Sokoni Na Kuwaibia Vitu Vyao Huko Cape Town,Sauz

Nyani wenye njaa kali wameleta hofu kubwa kwa wanawake ambao ni wakazi wa Jiji la Cape Town,South Afrika baada ya kuwavizia wanawake hao wakitoka sokoni na kuwaiibia vitu vyao kama mboga na vyakula vingine walivyonunua na kuwapora huku wengine wakijeruhiwa. Nyani maarufu katika eneo hilo kwa kuwaibia wanawake hao aitwaye Chacma Bides imeelezwa ni mtaalamu wa kuvizia na hukaa eneo la soko hilo muda wa mchana kusubiri wanawake wakitoka huwakimbiza na kuwanyang’anya mboga zao na kutokomea nazo.

Thursday, July 18, 2013

AUDIOS - PNC HARUDI KWA KASI AACHIA NGOMA MBILI KWA PAMOJA


Mkali katika gemu hapa Tanzania aliyewahi kutingisha na bado anaendelea kutingisha katika gemu la Bongo Flava mkali kutoka Mwanza PNC sasa amerudi tena kwa kasi na ngoma mbili kali akidhihirisha kwamba yeye ni msanii ambae hawezi kupotea na kipaji ni chake alichopewa na Mungu. Mkali huyo ambae yuko chini ya kampuni ya Mtanashati iliyo chini ya Juma na Musoma ameachia ngoma mbili, moja inatwa "Wewe" na nyingine inaitwa "Kaolewe benki" aliyowashirikisha wakali wawili katika gemu Juma Nature na Dogo Janja..Sikiliza ngoma hizo hapo chini..Big up yourself PNC.

Take care