Wednesday, November 9, 2016

UTAFITI: MIKOPO YA WANAWAKE HUTUMIWA NA WANAUME ZAO KWENYE ANASA.


Matokeo ya utafiti wa kuangalia changamoto za ufanyaji biashara kwa mwanamke Tanzania umebaini kuwa wanaume hutumia mikopo ya wake zao kwa matumizi mingine ikiwamo anasa na pombe.Utafiti huo uliofanyika kati ya Julai 30 na Agosti 12 mwaka huu, umetolewa jana mbele ya wajasirimali wanawake nchini kupitia mkutano wa Chemba ya Wanawake wajasiriamali nchini.Utafiti huo ulihoji wanawake 154,makundi tisa na maofisa wa taasisi zisizo za kiserikali katika kanda sita za Tanzania bara.

 Mtafiti na mwasilishaji wa utafiti huo ,uliojikita kuchambua na kutoa mapendekezo ya kumwezesha mwanamke,Ndasile Chamkunde amesema zinahitajika juhudi ili kumsaidia mwanamke kuongeza uwezo wake kibiashara.

"Changamoto nyingine ni mchakato mgumu wa kusajili biashara zao, nusu ya waliohojiwa ndio  wamejisajili.” amesemaAmesema asilimia 75 wanauza katika soko la Afrika Mashariki ila asilimia 78 wanauza kwa muda tu, elimu yao ni chini ya kidato cha nne, na asilimia 48 wanategemewa na watu sita kupitia biashara zao, "amesema Chamkunde ambaye pia ni muhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha UDSM.
#Mwananchi

Monday, November 7, 2016

TANESCO YAOMBA KUONGEZA BEI YA UMEME MWAKANI


Dar es Salaam. Mchakato wa kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya ombi la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) la kuongeza bei ya nishati hiyo kwa wastani wa asilimia zaidi ya 18.9 ifikapo mwaka 2017, unatarajia kuanza.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imeeleza kuwa Oktoba 4, mamlaka hiyo ilipokea ombi la mabadiliko ya bei ya umeme, hivyo unaandaliwa mkakati wa kukusanya maoni ya wadau wa nishati hiyo.

“Mikutano ya ukusanyaji maoni kuhusu bei inayopendekezwa na Tanesco itaanza Novemba 16 katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha, Dodoma  na kwa Dar es Salaam ni Novemba 23,” inaeleza taarifa hiyo.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni miezi saba tangu kutangazwa kwa bei mpya ya umeme iliyokuwa na punguzo la asilimia 1.5 hadi 2.4 sanjali na kuondoa tozo ya kuunganishiwa umeme ya Sh5,000 na gharama ya huduma kwa kila mwezi ambayo ilikuwa na Sh5,520.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema shirika hilo limefanya tathmini na kujiridhisha kuwa hakuna hasara itakayopatikana endapo bei hiyo itatumika.  #mwananchi

MKUU WA WILAYA HAKABIDHI TV (RUNINGA)GEREZA LA TUNDURU

Mkuu wa wilaya ya Tunduru mh Juma Zuberi Homera ametimiza ahadi yake aliyotoa mara baada ya kuteuliwa na kulitembelea gereza la Tunduru kuwa atawapa wafungwa Runinga(TV) ili waweze kuona habari mbalimbali kwani ni haki yao kikatiba

Na TV yenyewe ndio hiyo hapo kama inavyo onekana katika picha

Friday, November 4, 2016

SEPETU NA MUNA KUVUANA NGUO

Maneno ya wemasepetu -  Rose Alphonce Nungu... Nakuita tena kwa mara ya pili Rose Alphonce Nungu.... Unanitafutia nini wewe mwanamke...!?

Nini nimekukosea wewe dada...? Niliapa na Miungu yote siwezi kupost kitu chochote kwa account yangu kinachokuhusu wewe ila wallahy wewe dada You are pushing my buttons...

Tena una push buttons zangu kikweli kweli cuz nimekaa kimya na yako mengi.... Usijisahaulishe leo nimekuja kwako na ukalia mno kutaka vitu visitoke kwenye mitandao...

Sasa nakwambiaje Rose, mimi sitovitoa mitandaoni cuz im nat dat illiterate kama wewe... But nataka kukuuliza kitu, kwanini unamfanya mama angu kama ndondocha wako...?

Let me tell u one thing, Rose, I have been in the industry kwa miaka 10, Never have I taken my mum kwenye sehemu za starehe tena usiku wa manane... Ntamuita mama angu pale ninapojua kuwa uwepo wa mam unahitajika kwenye hafla hii... Umekuja ukaamua kujiweka karibu na mama angu kiasi cha kwamba mimi tena nikawa sio shoga ako bali mama angu ndo ukamtawala.... Ulikuwa una yako...

Leo hii umeweza kumteka mama angu kiasi cha kwamba unamfanya ajione yuko age sawa na wewe... Mama angu ni wa kwenda mango garden jamani? sijawahi... Mama angu ni wa kukaa mpaka usiku wa manane kwenye wanja za starehe? Sijawahi.. Mama angu leo hii ni wa kumlisha maneno ya uongo na kweli akaonekana mbele ya binaadam ananikana mtoto wake wa kumzaa...?

Muna ulichomfanya mama angu Mungu ndo anajua na ipo siku isio na jina basi atakuadhirisha ila kaa ukitambua watoto wake wote hatupendi... So back to topic ya leo, umeona uendeleze ushenzi wako kwa kuanza kutunga uongo kwa watu wangu wa karibu... kama ulivyotangaza kwenye magroup yako kuwa unanipa mabwana...

Hivi Rose, mimi leo hii wewe unitaftie bwana kwakuwa wewe hutaki mabwana wa maana... Honey mimi sitafutiwagwi bwana... Mabwana wananitongoza wenyewe na mara nyingi nakuwa na mtu ninaempenda sio niliotafutiwa... Mimi sio mtoto mdogo...

Sasa naona umeanza na @junaithar kesho na kesho kutwa usiwasahau @directorjoan na @sweetlorah ... Afadhali hawa dada zangu naweza kuwapostia hata biashara zao na wakanilipa ... Niambie nini umefanya kwangu wewe.. Umenidhulumu

Tuesday, October 25, 2016

Mabadiliko yanayokuathiri wewe mwajiriwa na Ajira yako


Kwa Tanzania sasa hivi kupoteza kazi yako ni rahisi sana. Unaweza kwenda kazini leo ukakuta umefukuzwa.

Teknolojia inabadilisha kila kitu. Baada ya muda mfupi unaweza kukuta kazi yako inafanywa na mashine.

Kumbuka Sikwambii haya kukutia hofu ni Ukweli ili ujiandae Lolote laweza kutokea.

Mambo uliyokua huyajui:-

• Hakuna Tajiri alieajiriwa,matajiri wote wanamiliki biashara zao wenyewe. Usifikiri kuwa tajiri kwa kupitia kwenye ajira.

•  Huwezi kua tajiri kwa kutegemea mshahara wako anza sasa kufikiria na kufanya, buni mfumo utakaokutengenezea kipato wakati upo kwenye ajira kipato hicho kikizidi mshahara na fanya mpango uache kazi.

•  Kama hujui ni kwamba boss wako hana mpango wa kubadili maisha yako furaha yake yeye ni aone unamfanyia kazi kwa bidii. Ukiumwa leo ukabaki nyumbani miezi mitatu ukirudi kazini utakuta nafasi yako imeshachukuliwa.

•  Haijalishi una elimu kubwa kiasi gani au ndogo kiasi gani mwajiriwa ni mwajiriwa tu wote wana hatari moja/wote wanamfanyia kazi mtu, ukifukuzwa kazi leo maisha yako lazima yatayumba.

•  Kilio kimoja cha kila mwajiriwa ni mishahara haikutani. Unaweza kubadili hali hiyo leo kwa kua na mfumo wako unakutengenezea pesa nje ya ajira.

•  Usipoteze muda kuomba uongezewe mshahara au upande cheo waza kumiliki biashara yako mwenyewe.

•  Mshahara ukiongezeka ujue utatakiwa ufanye kazi nyingi zaidi/uzalishe Zaidi, ukipanda cheo ujue na majukumu yatakua mengi Zaidi. Pesa utakayoongezewa huwezi kuifurahia tena.

•  Kwenye mfumo wako mwenyewe ni kwamba kuna wakati utakua haupo lakini pesa zinaendelea kutengenezwa.

•  Kama unafarijiwa na mafao utakayopata uzeeni piga mahesabu ni kiasi gani utapokea na uone jinsi gani unapoteza muda.

•  Mafao unayoyasubiria baada ya miaka 40 ya ajira ungeweze kutengeneza mara 50 yake na kwa muendelezo yaani hiyo miaka 40 ya ajira ni miaka 5 tu inaweza kukufanya wewe uanze kuishi maisha ya kipato kinacholingana na mafao yako.

•  Ajira yako haikulindi bali inakufanya uwe mtumwa unauza muda na nguvu zako kila siku kipato ambacho siku zote hakitakaa kikutoshe.

•  Sikwambii haya ili uache kazi leo lah! Anza kujitengenezea mfumo leo ili undoke hapo bila maumivu wala hofu yeyote.

•  Zipo biashara nyingi za kuanza ukiwa kwenye ajira lakini changamoto kubwa ni kwamba zitakukosa wewe kwasababu upo kwenye ajira hivyo ukuaji wake utakua kwenye hatari kubwa sana.

•  Lakini zipo biashara ambazo unaweza kutenga ule muda wako wa ziada baada ya ajira ukawa unaikuza biashara hii na ikakuletea mafanikio makubwa sana.

Inawezekana wewe hujawahi kufikiria kua tajiri au kumiliki mali nyingi biashara zako na kadhalika lakini kujiajiri au kuwa na kipato cha ziada ni kitu cha muhimu kwa maana unakua hutegemei mshahara peke yake. Lolote linaweza kutokea kipindi hiki.

Kuwa makini na jitengezee njia za kukisaidia kabla mabaya hayajakufikia.

Mifumo ipo,

Tafakari, Chukua hatua
Huku ukimtanguliza Mwenyezi Mungu mbele.

VISA VYA WANAWAKE NA KUPONEA KUFA CHUPUCHUPU

NINGEKUFA KWA AJILI YA  MWANAMKE!!

Leo nimepita kisimani nikamkuta dada mmmoja akifua. ,Nikamuuliza eti dada unavijua visa vya wanawake??

Akajibu kaka niache, nikakomaa anijibu...
Badala ya kujbu akaanza kupiga mayowe, na kelele za kuomba msaada.. hadi wananchi wenye mapanga, mawe na mishale wakaanza kuja, dada huyo alivyoona wanakuja akajmwagia maji mwili mzima. Nikajua leo ndio mwisho wangu nikajuta sana kutaka kujua kila kitu..

Wananchi walivyofika, wakamuulza, kuna nini? Akawajibu, nilidumbukia kwenye kisima na huyu kaka ndie amensaidia!!
Wakanipongeza sana sana kisha wakaondoka...

Yule dada  akaniambia, hivyo ndivyo visa vya mwanamke anaweza kukuua au kukulinda! So muheshmu mwanamke hata kinafiki, usijfanye jeuri!!!

*KUOLEWA NI NDOTO KUU YA KILA MWANAMKE ALIYEKAMILIKA ILA KAMA UNA TABIA HIZI UTAZEEKEA NYUMBANI*


*1. Tamaa ya utajiri* fedha na mali nyingi pasipo kutambua kuwa vitu hutafutwa, hapa wengi hupoteza nyota zao kwa kukataa wengi wenye kipato cha kawaida na kujirahisisha kwa wenye nazo ambao kwa bahati mbaya wengi wao sio waoaji bali ni wahuni tu na watu wa anasa na kula bata mjin.

*2. Dharau,* maringo, kiburi na mashauzi yaani we kila mtu akikusogelea na kujaribu kuzungumza na wewe unaanza kumpandisha na kumshusha kisha una msonya. Wengi huishia kukupotezea wakijua either umewadharau au tayari una mtu wako ndio maana nyodo nyingi.

*3. Husali* hakika lazima wahuni watapata nafasi kwako na kukuchezea mpaka uchakae kama mtumba wa uvira. MWENYEZI MUNGU ndo  anaetoa BARAKA ukimuomba hakika atakuepushia kuingia midomon mwa dubu na fisi wanaokuwa wakikuvizia na kuja kama MALAIKA. Atakupa ufahamu wa kuwatambua na kuwashtukia mapema.

*4. Kuvaa nguo za ajabu ajabu kama changudoa*
. Sijui ni nani aliyewaambia kuwa mkivaa hivyo mnapendeza! Unakuta binti unavaa kama mcheza show za Casino yaani ukipita nguo yaonyesha kila kitu ukiinama ndio balaa kabisa yaani kimin kinafunuka kila kitu nje nje kwa style hiyo nani atakupeleka kwao?

*5. Kujipaka marangi ya ajabu ajabu usoni kama mwali wa kibembe*
au kizaramo kwanza mnatutisha tu.

*6. Kupenda kujirahisisha au kujipendekeza pendekeza kwa wanaume,*
yani ukiguswa kidogo tu twende.

*7. Kuwa na picha karibia 500 Facebook,* Twitter nk halafu picha zenyewe hazieleweki yani zimepigwa katika mavazi au mapozi ya ajabu ajabu, mara umebinua makalio, mara tumbo, mara mdomo,

*8. Kila unachofanya basi unakimbilia kupost mfano kwenye Facebook* na kadhalika
nyinginezo hata ukienda haja basi lazima upost.

*9. Ni mtu wa maneno maneno*
yani we kila unachokiona unaongea na kuropoka ropoka tu hauna break! mwanamke gani?

*10. Huna mawazo ya malengo* endelevu yani we kwenye kichwa chako kumejaa umbea tu sijui leo Wema Sepetu amefanya nini? Sijui Kim, Lupita amefanya vile na upuuzi mwingine.

*11 Mizinga.*
Yani siku ya pili tu baada ya kukutongoza unaanza " honey nataka galaxy" Htc" Huawei" mara baby nimeona nguo nzuri mara ooh baby yaani njaa inauma'' , utasindikiza harusi za wenzio hadi upigwe alama..

Waswahili husema, "Kama mzuri, Olewa"

Jihadhari na tabia hizi.
_Maneno makali ila ujumbe umefika.