Wednesday, November 9, 2016

UTAFITI: MIKOPO YA WANAWAKE HUTUMIWA NA WANAUME ZAO KWENYE ANASA.


Matokeo ya utafiti wa kuangalia changamoto za ufanyaji biashara kwa mwanamke Tanzania umebaini kuwa wanaume hutumia mikopo ya wake zao kwa matumizi mingine ikiwamo anasa na pombe.Utafiti huo uliofanyika kati ya Julai 30 na Agosti 12 mwaka huu, umetolewa jana mbele ya wajasirimali wanawake nchini kupitia mkutano wa Chemba ya Wanawake wajasiriamali nchini.Utafiti huo ulihoji wanawake 154,makundi tisa na maofisa wa taasisi zisizo za kiserikali katika kanda sita za Tanzania bara.

 Mtafiti na mwasilishaji wa utafiti huo ,uliojikita kuchambua na kutoa mapendekezo ya kumwezesha mwanamke,Ndasile Chamkunde amesema zinahitajika juhudi ili kumsaidia mwanamke kuongeza uwezo wake kibiashara.

"Changamoto nyingine ni mchakato mgumu wa kusajili biashara zao, nusu ya waliohojiwa ndio  wamejisajili.” amesemaAmesema asilimia 75 wanauza katika soko la Afrika Mashariki ila asilimia 78 wanauza kwa muda tu, elimu yao ni chini ya kidato cha nne, na asilimia 48 wanategemewa na watu sita kupitia biashara zao, "amesema Chamkunde ambaye pia ni muhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha UDSM.
#Mwananchi

Monday, November 7, 2016

TANESCO YAOMBA KUONGEZA BEI YA UMEME MWAKANI


Dar es Salaam. Mchakato wa kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya ombi la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) la kuongeza bei ya nishati hiyo kwa wastani wa asilimia zaidi ya 18.9 ifikapo mwaka 2017, unatarajia kuanza.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imeeleza kuwa Oktoba 4, mamlaka hiyo ilipokea ombi la mabadiliko ya bei ya umeme, hivyo unaandaliwa mkakati wa kukusanya maoni ya wadau wa nishati hiyo.

“Mikutano ya ukusanyaji maoni kuhusu bei inayopendekezwa na Tanesco itaanza Novemba 16 katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha, Dodoma  na kwa Dar es Salaam ni Novemba 23,” inaeleza taarifa hiyo.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni miezi saba tangu kutangazwa kwa bei mpya ya umeme iliyokuwa na punguzo la asilimia 1.5 hadi 2.4 sanjali na kuondoa tozo ya kuunganishiwa umeme ya Sh5,000 na gharama ya huduma kwa kila mwezi ambayo ilikuwa na Sh5,520.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema shirika hilo limefanya tathmini na kujiridhisha kuwa hakuna hasara itakayopatikana endapo bei hiyo itatumika.  #mwananchi

MKUU WA WILAYA HAKABIDHI TV (RUNINGA)GEREZA LA TUNDURU

Mkuu wa wilaya ya Tunduru mh Juma Zuberi Homera ametimiza ahadi yake aliyotoa mara baada ya kuteuliwa na kulitembelea gereza la Tunduru kuwa atawapa wafungwa Runinga(TV) ili waweze kuona habari mbalimbali kwani ni haki yao kikatiba

Na TV yenyewe ndio hiyo hapo kama inavyo onekana katika picha

Friday, November 4, 2016

SEPETU NA MUNA KUVUANA NGUO

Maneno ya wemasepetu -  Rose Alphonce Nungu... Nakuita tena kwa mara ya pili Rose Alphonce Nungu.... Unanitafutia nini wewe mwanamke...!?

Nini nimekukosea wewe dada...? Niliapa na Miungu yote siwezi kupost kitu chochote kwa account yangu kinachokuhusu wewe ila wallahy wewe dada You are pushing my buttons...

Tena una push buttons zangu kikweli kweli cuz nimekaa kimya na yako mengi.... Usijisahaulishe leo nimekuja kwako na ukalia mno kutaka vitu visitoke kwenye mitandao...

Sasa nakwambiaje Rose, mimi sitovitoa mitandaoni cuz im nat dat illiterate kama wewe... But nataka kukuuliza kitu, kwanini unamfanya mama angu kama ndondocha wako...?

Let me tell u one thing, Rose, I have been in the industry kwa miaka 10, Never have I taken my mum kwenye sehemu za starehe tena usiku wa manane... Ntamuita mama angu pale ninapojua kuwa uwepo wa mam unahitajika kwenye hafla hii... Umekuja ukaamua kujiweka karibu na mama angu kiasi cha kwamba mimi tena nikawa sio shoga ako bali mama angu ndo ukamtawala.... Ulikuwa una yako...

Leo hii umeweza kumteka mama angu kiasi cha kwamba unamfanya ajione yuko age sawa na wewe... Mama angu ni wa kwenda mango garden jamani? sijawahi... Mama angu ni wa kukaa mpaka usiku wa manane kwenye wanja za starehe? Sijawahi.. Mama angu leo hii ni wa kumlisha maneno ya uongo na kweli akaonekana mbele ya binaadam ananikana mtoto wake wa kumzaa...?

Muna ulichomfanya mama angu Mungu ndo anajua na ipo siku isio na jina basi atakuadhirisha ila kaa ukitambua watoto wake wote hatupendi... So back to topic ya leo, umeona uendeleze ushenzi wako kwa kuanza kutunga uongo kwa watu wangu wa karibu... kama ulivyotangaza kwenye magroup yako kuwa unanipa mabwana...

Hivi Rose, mimi leo hii wewe unitaftie bwana kwakuwa wewe hutaki mabwana wa maana... Honey mimi sitafutiwagwi bwana... Mabwana wananitongoza wenyewe na mara nyingi nakuwa na mtu ninaempenda sio niliotafutiwa... Mimi sio mtoto mdogo...

Sasa naona umeanza na @junaithar kesho na kesho kutwa usiwasahau @directorjoan na @sweetlorah ... Afadhali hawa dada zangu naweza kuwapostia hata biashara zao na wakanilipa ... Niambie nini umefanya kwangu wewe.. Umenidhulumu