Tuesday, December 8, 2015

KIJANA KIONGOZI MWANAHARAKATI

Malila machim @malilerlovedejo apata dili ya kuwa mmoja wa wanachama na mwanaharakati wa watu wenye ulemavu wa ngozi au ualbino mkoa wa morogoro.

LEVEL ZA MVULANA BOYA NI

1. Kama umetembelewa na demu ile ameingia chumbani kwako tu mmekaa muda mara anakwambia funga mapazia na mlango alafu akawasha sabufa kwa sauti ya juu na wewe ukakaa kama zezeta unashangaa ka uko feri huo ni uboya na wewe una MSINGI mzuri wa uboya. 2 Kama upo na demu geto mnacheki movie alafu anakwambia yupo bored hainjoi hiyo movie unamwambia uweke nyingine anakataa unamuuliza anataka nini anakutizama machoni anatabasamu kidogo wewe huelewi ufanyaje unaenda kutafuta CD ya movie ya Rambo jua wewe ni boya level ya SECONDARY yaani hapo ni A ya uboya unasubiri kwenda Chuo 3. Upo na demu getto mmechili mnampigishana story za hapa na pale mara anakuambia kuna kitu anatakitamani kwa siku hiyo wewe huelewi hata tone ndio kwanza unakazana kumuonesha picha zako za shule ya msingi yeye anakwambia anataka kuondoka unaendelea kumuonesha sijui picha kwenye gallery yako na yeye kila mara anakuambia anataka kuondoka na wewe hujiongezi hujui anamaanisha nini basi jua wewe ni boya mimi nakutunuku CERTIFICATE ya UBOYA 4. Kama upo na demu getto kwako kwenye sofa mnapiga story na kucheki series ya Vampire Daries akakwambia uitoe uweke CD yeyote ile ambayo ni romantic ukamuwekea mkaangalia akawa anainjoi sana ghafla akatoka kwenye sofa na kujitupa kitandani alafu akakwambia mlale huku mkipiga story wewe ukaenda na kuanza kumsimulia hadithi za Sungura na Fisi Mara alifu lela uliwe basi umeshaufaulu mtihani wa Uboya na umepewa DEGREE yake

Sunday, October 4, 2015

TABIA YA WATU WASIO NA MAFANIKIO

1. Ni watu wenye tabia ya kujipendelea wao wenyewe, watu wenye umimi na ubinafsi wakati wote 2. Ni watu wenye tabia ya ubishi na kupinga kila jambo, hususani lile ambalo mwingine amelisema ama kulizungumza, kwao hoja ya mwingine sio hoja bali hoja yao ndiyo hoja pekee. 3. Ni watu wenye visasi na mafundo ya moyoni hata katika vitu vidogo na visivyo vya msingi, wanaweza kuzira kirahisi tena kwa muda mrefu bila hata sababu ya msingi 4. Wanaumizwa sana pale mwingine anapopewa pongezi au kusifiwa au kupewa ushindi, kiu yao ni kwamba pongezi zote na sifa zote na ushindi wote uwe wakwao. Mara mwingine anapoonekana kushinda basi wao hujifanya ndio waliokuwa chachu au wasababishaji wa ushindi huo na kwahivyo wanataka wapongezwe wao au mchango wao kukubalika mbele za watu 5. Ni watu walalamishi sana na wenye kulaumu kila mazingira, huwalaumu wengine pale wao wanapoonekana kushindwa, wakishindwa au kufeli wao basi huzitupia lawama kwa watu wanaowazunguka, utasikia wakisema “kama asingekuwa fulani basi nisingeshindwa hivi, yeye ndiyo amesababisha mimi kufeli au kutofanya vizuri” 6. Wanapenda na wala hawaoni tatizo kupoteza muda, anaweza kukaa mbele ya televisheni masaa na masaaa bila kujali muda unavyopotea 7. Mara nyingine hujaribu kujiwekea mpangilio wa siku wa nini atafanya na wakati gani lakini kamwe hawawezi kufwata walichokipanga wenyewe 8. Ni waoga na wapinzani wa mabadiliko hata kama hawanauhakika nini asili ya mabadiliko hayo 9. Mara zote hudhani na hufikiri kuwa wanajua kila kitu, ni ngumu sana kuishi na mtu wa aina hii kwa maana wakati wote ni ngumu kumbadili au kubadili lile analoliwaza au kulifikiri maana yeye anauhakika kuwa anafahamu kuliko mwingine yeyote 10. Katika kila wanalofanya wao husukumwa na mawazo au kiu ya kujua nini anafaidika nacho, kama yeye hapati manufaa ya moja kwa moja katika chochote afanyacho basi hawezi kushiriki chochote. Watu wahivi ni ngumu sana kusaidia mtu mwingine au kutoa mchango wa hali na mali kwa jamii maana wao huona kuwa hauna faida za moja kwa moja kwake. 11. Ni watu wanaopenda kuwazungumzia wengine, huzungumzia madhaifu ya watu na kushindwa kwa wengine, hata siku moja hawawezi kujadili mafanikio ya mtu mwingine 12. Mara nyingi ndani ya mioyo yao huwaza au kutamani wengine washindwe au wasiendelee, tena sio kutamani tu bali huumia wanapoona wengine wanafanikiwa 13. Sio wepesi wa kutoa taarifa muhimu kwa wengine, ni wafichaji wa taarifa za muhimu maana ndani yao wanakiu ya kuzuia maendeleo yaw engine au kuona wengine wanafanikiwa 14. Hawafahamu wala hawajui nini wanatamani wala ni nini wanataka maishani, kwa maana hiyo ni ngumu kufikia katika mustakabali wowote 15. Ni watu wenye hasira au kushindwa kujizuia kuonyesha hasira zao 16. Ni watu wasio na malengo, wasioweka malengo binafsi na wala hawawezi kuyafuata malengo yao, kwa hali hiyo basi inakuwa ngumu kufikia mafanikio maishani mwao.  

Saturday, October 3, 2015

TABIA ZA WATU WALIO FANIKIWA

Kufanikiwa ni kiu ya kila mmoja ingawa ukweli ni kwamba wengi wetu tunabaki tunayatamani mafanikio wakati hatuna mazingira yeyote ya kuruhusu mafanikio hayo yawepo au yatujie. Hapa nakuletea tabia za watu wawili tofauti, mmoja akiwa ni mtu mwenye mafanikio au yule ambaye ana mazingira ya kuja kufanikiwa na mwingine ni mtu asiye na mafanikio na asiye na mazingira ya kufanikiwa maishani. Nitaanza na tabia za watu wenye mafanikio; 1. Ni watu wenye kushukuru kwa kila jambo, sio wenye kutoa lawama 2. Ni watu wenye tabia ya kupongeza pale wanapoona mwingine anastahili pongezi 3. Ni watu wenye tabia ya kusamehe, tena wanasamehe kwa urahisi wala sio kwa kuombwa na kulazimishwa 4. Ni watu wasioona uchungu kuwapongeza wengine au kukubali wengine wanapopata ushindi wa aina yeyote, na sio tu kuwapongeza bali pia hawaoni ugumu kuwasaidia au kuwashauri wengine ili wafanikiwe zaidi 5. Ni watu wanaokubali wakati wote kubeba majukumu au lawama pale wanaposhindwa kufanya inavyopaswa, sio wenye kujitetea au kujaribu kukwepa majukumu 6. Ni watu wenye tabia ya kupenda kusoma kitu kila siku, sio wavivu wa kusoma au kutafuta taarifa na ujuzi 7. Ni watu wenye tabia ya kuweka utaratibu wa nini kinafanyila leo na nini kitafanyika kesho na kwa nini kifanyike, sio watu wanaoburuzwa na mazingira yanaowazunguka au kuendeshwa na marafiki zao 8. Sio watu wenye kuzungumza sana kuhusu watu wengine na madhaifu yaw engine bali ni wenye kuzungumza zaidi kuhusu mawazo ya kujenga au mawazo ya kimaendeleo 9. Mara zote wana kiu ya kuona wengine wanafanikiwa, hata kama mafanikio hayo yatayazidi yale wao walionayo 10. Sio wachoyo katika kutoa taarifa au ujumbe wowote muhimu kwa mtu yeyote, maana wao hawana uchungu na mafanikio au ushindi wa mwingine 11. Ni watu wenye kuonyesha furaha wakati wote, sio wenye kununa, kuzira na kuwa na huzuni mara kwa mara 12. Ni watu wanaoweka malengo na kuongozwa na malengo katika maisha yao ya kila siku, sio wanaokurupuka kufanya mambo kwa hisia, misukumo au mashindano tu 13. Sio waoga wa mabadiliko, bali hutamani mabadiliko chanya na yenye kujenga na kuleta maendeleo, na kwahiyo mara zote kuyawezesha mabadiliko kutokea kwao na kwenye maisha ya wengine na sio kuyapinga 14. Kwao kujifunza ni tabia endelevu sio jambo linalotokea wakati wakiwa shuleni tu, wao huhesabu maisha ya kila siku ni kama shule 15. Kiu na msukumo wa maisha yao ya kila siku ni katika kusababisha mabadiliko, aidha mabadiliko kwao wao binafsi au kwa wale wanaowazunguka.  

ILI UFANIKIWE UNAHITAJI UWE NA TABIA HIZi

NIMEKUBAMBA

MAMBO KUMI YA KUFURAHISHA NA HUWEZI KUYAFANYA: 1. Huwezi kuosha Macho kwa Sabuni 2. Huwezi kuhesabu Nywele zako 3. Huwezi kupumua kwa Pua na huku umetoa Ulimi 4. Unajaribu kufanya namba 3 6. Umeona inawezekana, sanasana unakuwa Kama Jibwa 7. Unatabasamu kwa kuwa umejiona Mjinga! 8. Umeruka namba 9. Unahakikisha Kama kweli 5 haipo. 10. Unacheka kwa kuwa nimekubamba! Shea na wenzako na wewe uwabambe! 😆😆😆😆😆

MUME MPENDA UGOMVI

**MUME MPENDA UGOMVI** Kila siku akirudi nyumbani hutafuta vijisababu visivyo na msingi......... Siku hiyo mke akajitahidi kuweka mazingira safi. Sebuleni pakafagiliwa kufutwa na kupangwa vizuri, Chumbani kila kitu safi, Watoto wameogeshwa wanang'aa, Mke kajipamba kama siku ya harusi. Mume kuingia akaangaza huku na huko kila kitu poa, Kukaa kwenye kochi...mara akafoka.... "Mama Abdallah! Mama Abdallah!" Mke: Labeika Mume wangu! Mume: Liko wapi lile vumbi lilokuwa hapa kwenye coffee table?? Mke: Si nimelifuta mume wangu kwani kuna nini Mume: Kuna namba ya simu muhimu nilikuwa nimeandika juu yake!! Mke: mmmmhh!! Baba Abdallah!!! 😂😂😂😂😂

HARAKATI ZA KUFUNGA KAMPAINI UTAYAONA HAYA USISHANGAE

1.Television ya taifa na zingine washirika kumuonesha mwalimu Nyerere mara nyingi zaidi ya siku za nyuma wakiweka hotuba zisizoponda chama tawala lakini zikikaa mrengo wa kukitetea haya yatafanyika kuelekea 14 October kwenye kumbukumbu ya mwalimu 2. Umeme kuwepo siku nzima na nchi nzima siku zifuatazo siku CCM itakapoenda Mwanza na mikoa mingine mikubwa ili watu waweze kuona na kusikia mikutano yao live nchi nzima lakini mgao utaendelea siku wapinzani wap wangu wakipita mikoa hiyo hiyo either wakiwa wametangulia au baadaye. 3. Kukamatwa kwa kiongozi mkubwa wa chama kimoja kwa kosa lililompeleka mbasha au babu seya kortini na kutangazwa sana na vyombo vya habari ikiwemo kuwaweka wazi waathirika wa tukio hilo litapotokea kesi itaisha baadae baada ya uchaguzi. 4. Kulazimishwa kwa kuombwa sana kwa mke wa kiongozi wa kitaifa anayeheshimika kutoa tamko siku ya kilele cha maadhimisho ya marehemu mumewe kwa hotuba fupi itakayoandaliwa au mahojiano yatakayoandaliwa kuonesha kwamba fulani sio chaguo na mengineyo. 5. Kukamatwa kwa watu watakaokuwa na Silaha za kivita wakiitwa"magaidi wenye mafunzo ya kikomandoo"ambao watasema wameletwa na chama kimoja cha siasa kwa shughuli maalumu .kumbuka hawatakuwa watanzania watatoka nchi inayosifika kwa magaidi afrika . 7. Kujitoa au kushawishiwa kujitoa kwa chama kimoja au kiongozi wake mkuu kwa madai ya kutotendewa haki na muungano wao.  8.Wagombea urais wawili au watatu kutangaza kumuunga mkoani mgombea wa chama kingine na Hii wataifanya hadharani siku ya kufunga kampeni kwa hicho chama. 9.Siku ya ufungaji wa kampeni tutashuhudia mwenyekiti wa chama kimoja wenye mamlaka ki nchi akimtuhumu waziwazi na kumtaja jina mgombea wa chama pinzani na washirika wake wakuu kuhusika na ufisadi uliotajwa sana tukio hilo litafanyika na kuoneshwa live na TV na redio nchi nzima na kupewa uzito kwenye magazeti yote kesho yake. Lakini siku inayofuata ambayo chama tuhumiwa kitataka kujibu mapigo umeme utakatika nchi nzima so hawatakuwa live zaidi ya uwanjani pia magazeti ya siku ya uchaguzi yatawekewa oda ya jumla na tutayapata jioni au tusipate kabisa yatakuwa yameandika habari hizo za kufunga kampeni na majibu ya tuhuma kwa uwazi na vielelezo lakini itakuwa too late. 10. Uchaguzi utagubikwa na fujo kwa karatasi kuchelewa Vituoni, polisi kutumia nguvu kubwa,watu kuvaa tishet za vyama wasivyoshabikia na kufanya vurugu ila tishet hzo ni mpyaaaa. Baadhi ya vituo watu hawatapiga kura uhesabu wa kura kielectonic utaleta utata mkubwa kwa kutofautiana na uhalisia wa jumla ya kura zote. Kurudiwa kura sehemu mbalimbali kwa sababu mbalimbali. Kukamatwa kwa wapiga kura mamluki au wanaotaka kutumika kupigia MENGINE NITALETA BAADAYE USINIBISHIE KAA UTICK KILA KITAKACHOTOKEA KUTOKANA NA MUDA KAMA NI MDAU CHUKUA TAHADHARI

Tuesday, March 17, 2015

NEWS | Imetosha Movement Kufanya Matembezi Hisani Machi 28

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya taasisi ya ‘Imetosha Movement’ na viongozi wakizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni. ASASI ya Harakati za Imetosha ilioanzishwa kupinga mauaji na vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watu wenye u-albino inatarajiwa kufanya matembezi makubwa ya hisani kuchangisha fedha kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu kwa uma juu ya imani potofu zinazoendelea za mauaji ya albino. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Kujitolea wa Harakati za ‘Imetosha Movement’, Henry Mdimu amesema matembezi ya hisani kuchangia fedha zitakazowezesha kutolewa kwa elimu kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa juu ya imani potofu zinazoendelea na mauaji ya albino yanatarajia kufanyika Dar es Salaam Machi 28, 2015. Alisema matembezi hayo yataanzia katika Viwanja vya Leaders na kuzunguka maeneo yaliyopangwa kisha kurejea viwanjani hapo kwa ajili ya shughuli maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya harakati maalumu za imetosha zitakazo kwenda kwa jamii ya kawaida na kueneza elimu ikiwa ni juhudi za kuhamasisha kila mwana jamii kupaza sauti na kusema ‘Imetosha Mauaji ya Albino’. “…Baada ya taratibu kukamilika, matembezi sasa yatafanyika Tarehe 28 Machi kuanzia saa 12 Alfajiri, kutoka Leaders Club tutazunguka na kurudi hapo, karibuni sana tuchangie harakati hizi zenye lengo zuri kwa mustakabali wa Taifa letu lenye sifa ya amani na utulivu,” alisema Mdimu katika taarifa yake. Aidha akizungumzia uvumi ulioenea hasa katika nchi za nje, unaodai kwamba serikali imekataza watu wenye ulemavu wa ngozi kuandaa matembezi au maandamano alisema taarifa hizo hazina ukweli wowote na kuongeza kuwa kuna taratibu za kufuata kabla ya uandaliwa shughuli hizo. “…Hili suala sio kweli, ili ufanye mambo kama haya ni lazima upitie taratibu za kisheria ili upate kibali. Hii ni nchi na ina taratibu zake kwa hiyo tulipaswa kuzifuata na ndio kilichosababisha hata matembezi yetu kuahirishwa. “Tulikuwa tunafuata taratibu na leo rasmi tumepata usajili wa Imetosha…sasa imetosha imekuwa taasisi kamili inayoitwa IMETOSHA MOVEMENT. Napenda kuchukua wasaa huu kuwashukuru marafiki wote wanaoniunga mkono, na kunipa moyo, msinichoke kwa sababu safari bado ni ndefu,” Hata hivyo aliwataka wananchi na wadau mbalimbali yakiwemo makampuni kujitokeza katika matembezi hayo ya hisani ili kuunga mkono juhudi sa mapambano ya kukomesha mauaji na vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa watu wenye ualbino maeneo mbalimbali ya nchi.