Saturday, October 3, 2015

MUME MPENDA UGOMVI

**MUME MPENDA UGOMVI** Kila siku akirudi nyumbani hutafuta vijisababu visivyo na msingi......... Siku hiyo mke akajitahidi kuweka mazingira safi. Sebuleni pakafagiliwa kufutwa na kupangwa vizuri, Chumbani kila kitu safi, Watoto wameogeshwa wanang'aa, Mke kajipamba kama siku ya harusi. Mume kuingia akaangaza huku na huko kila kitu poa, Kukaa kwenye kochi...mara akafoka.... "Mama Abdallah! Mama Abdallah!" Mke: Labeika Mume wangu! Mume: Liko wapi lile vumbi lilokuwa hapa kwenye coffee table?? Mke: Si nimelifuta mume wangu kwani kuna nini Mume: Kuna namba ya simu muhimu nilikuwa nimeandika juu yake!! Mke: mmmmhh!! Baba Abdallah!!! 😂😂😂😂😂

No comments:

Post a Comment