Friday, August 5, 2016

LISSU AFIKISHWA TENA MAHAKAMANI

Dar es Salaam. Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu amefikisha Mahakamani  ya Kisutu saa  8. 46  huku mahakamani hapo kukiwa na ulinzi mkali.

Ulinzi umeimarishwa katika mahakamani hapo muda mrefu wakati wakimsubiria Lissu akitokea katika kituo cha polisi kanda maalumu.

Polisi wapatao tisa baadhi ya wakiwa na silaha  wametanda katika eneo la mbele la mahakama hiyo.

HOMA YA MANJANO: WHO LAWAMANI


Uchunguzi wa shirika la habari la AP umebaini kwamba shirika la afya duniani WHO lilitekeleza makosa makubwa katika kukabiliana na mlipuko wa homa ya manjano Afrika ya Kati.

Uchunguzi huo unasema chanjo milioni moja zilizokuwa zikisafirishwa hadi Angola zilitoweka kutoka kwenye shehena ya chanjo milioni sita za homa hiyo ya manjano.

Baadhi ya chanjo zilipelekwa katika maeneo ambayo hayakuwa yameathiriwa na homa hiyo, huku zilizopelekwa katika maeneo yaliyoathiriwa, zikikosa sindano.

#BBC

Wednesday, August 3, 2016

WAFANYAKAZI WA CHINA WASHAMBULIWA KENYA:


Kundi moja la vijana waliojawa na ghadhabu na ambao walikuwa wamejihami na fimbo waliwavamia raia wa Uchina wanaofanya kazi ya ujenzi wa barabara ya kisasa ya Treni nchini Kenya.

Wafanyikazi 14 wa China walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo katika eneo la Narok, takriban kikomita 200 kusini magharibi mwa mji wa Nairobi.

Washambuliaji hao walidaiwa kulalamikia kampuni ya kujenga barabara na madaraja ya China kwa kutowapatia ajira za ujenzi wa reli hiyo.

Makumi ya maafisa wa polisi wamepelekwa katika eneo hilo huku mamlaka ikifanya mikutano ya dharura kwa lengo la kutuliza hali.

Kuna Takriban raia 4000 wa China wanaofanya kazi nchini Kenya hususan katika viwanda vya ujenzi pamoja na biashara za kuuza vifaa vya kielektroniki.

#BBC

Tuesday, August 2, 2016

Trump asema Hillary Clinton ni 'shetani'

Trump asema Hillary Clinton ni 'shetani'

Mgombea wa chama cha Republican nchini marekani Donald Trump amemtaja mshindani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton kuwa 'shetani'.

Akizungumza kwenye mkutano huko Pennsylvania bwana Trump alimshambulia Bernie Sanders kwa kumuachia nafasi Bi Clinton.
Tajiri huyo alisema kuwa Sanders alifanya makubaliano na 'shetani'.

Wanachama wa Democrat na Republican wememkosoa bwana Trump kutokana na matamshi yake kuhusu wazazi wa mwanajeshi M'marekani muislamu aliyeuawa vitani nchini Iraq.

WAZIRI MKUU AYAKATAA MADAWATI YA TFS


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekataa kupokea msaada wa madawati uliotolewa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) baada ya kubaini yametengenezwa chini ya kiwango. “Ofisa elimu njoo kagua haya madawati yaliyo mazuri nitayapokea na yaliyobaki yarudishwe karakana yakatengenezwe upya huu si wakati wa kupokea vitu vibovu,“ amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo wakati alipowasili katika kiwanja cha Mabau, Mtibwa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ambapo alikabidhiwa madawati hayo na Meneja wa TFS.

Amesema anatambua dhamira ya TFS ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kumaliza tatizo la upungufu wa madawati lakini hawezi kupokea kupokea madawati yaliyotengenezwa chini ya kiwango.

AKATWA MIKONO KWA 'KUKOSA KUSHIKA MIMBA' KENYA:


Mwanamume mmoja nchini Kenya amedaiwa kumkata mikono yote miwili mkewe kwa kutumia kisu kikubwa kwa kushindwa kumzalia watoto,katika kile kinasemekana ni kisa kibaya zaidi cha ugomvi wa nyumbani.

Mikono ya Jackline Mwende kutoka kijiji cha Kathama ,Masii katika kaunti ya Machakos ilikatwa kutoka katika kifundo cha mkono na mumewe Stephen Ngila Thenge tarehe 24 mwezi Julai.

Pia ana majeraha katika kichwa chake na shingo kutokana na shambulio hilo.

Ndugu zake wanasema kuwa wanandoa hao walikuwa na matatizo na kwamba bi Mwende alitaka kumwacha mumewe,lakini akashauriwa kutofanya hivyo na kiongozi mmoja wa dini.

Mwende anasema kuwa kabla ya shambulio hilo walikuwa wakiishi mbalimbali na mumewe kwa takriban miezi mitatu kwa kosa la kutopata watoto. ''Sijui kwa nini aikuwa akinilaumu licha ya sisi sote kwenda hospitalini mwaka uliopita na kwamba daktari alisema kuwa ni yeye aliyekuwa na tatizo la kuzaa ambalo linaweza kurekebishwa''. Anasema kuwa mumewe ambaye ni mshonaji nguo katika mji wa Masii alikataa kufuatilia matibabu.

#BBC

Monday, August 1, 2016

MAANDAMANO: WATU 10 WAUAWA ETHIOPIA.

Makumi ya maelfu ya watu kutoka kabila la Amharic wameshiriki katika maandamano dhidi ya Serikali nchini Ethiopia katika mji wa kaskazini wa Gondar.

Waandamanaji hao wameitaka serikali kubadilisha uamuzi wake wa kuanzisha wilaya chini ya usimamizi wa kabila la Tigray.

Serikali ya Ethiopia inasema kuwa zaidi ya watu 10 wameuawa wakati wa makabiliano na polisi kuhusu eneo linalozozaniwa katika majuma ya hivi karibuni.

JIFUNZE WEWE MWANAMKE ULIYE SINGLE.

Tambua lengo lako kabla hujaingia kwenye ndoa.

Fanya biashara yoyote, tafuta shughuli ya kufanya.

Usimsubiri mwanaume ndio useme unaanza maisha.

Ongeza thamani ya maisha yako kwa kujenga maisha yako.

WALIMU MBARONI KWA KUNYWA POMBE SAA ZA KAZI

Sengerema. Baadhi ya walimu wa shule ya msingi Chifunfu katika Halmashauri ya Sengerema mkoani Mwanza wamekamatwa baada ya kukutwa wakinywa pombe saa za kazi.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Chifunfu, Lucas Mashinji amesema walimu hao walikutwa baa Julai 29 saa 3.15 asubuhi, baada ya raia wema kutoa taarifa kwa diwani wa eneo hilo, Robert Madaha.

Mashinji amesema walimu hao wanashikiliwa ofisi ya kata wakisubuiri taratibu nyingine kufanyika.

Diwani Madaha alisema taarifa za walimu hao alizipata kutoka kwa wananchi kuwa walimu hao wapo baa hivyo alitoa maagizo wakamatwe.