Thursday, October 13, 2016

MODELING INSPIRATION


Kila kinacho fanyika ndani ya maisha yetu ya kila siku kinaongozwa na nia,utayari,kujiamini,kujituma na kujisimamia"

Haiwezi kuwa rahisi mtu kutimiza ndoto zako katika maisha juu ya kile unacho kitazamia kama wewe mwenyewe haupo tayari kuona ndoto zako zikifanikiwa katika hilo :

Huyu ni model anayeishi South Africa .Ni model mwenye Albinism :

Hata siku moja hakutaka kuishi kwa kuikubali hali yake ya udhaifu wa ngozi,jamii inavyo mchukulia na jinsi hali nzima ya muonekano wake wa mwili ilivyo (Albino) ILA tangu akiwa na umri mdogo alijiandalia njia na mazingira mazuri ya kuiaminisha jamii kuwa anaweza na nimfano wa kuigwa :

Siku zote aliishi kwa kuamini yeye ni mshindi na nibora zaidi katika kila anacho kifanya kutetea ndoto zake za maisha kupitia modeling HAKURUHUSU hata siku moja mawazo na mitazamo ya watu wanao mzunguka viweze kumkatisha tamaa na kujihisi hana tena thamani katika dunia ya kuishi maisha ya ndoto zake:

Daima alitia nia na kujituma zaidi katika kuutafuta ushindi wa mawazo,uhuru,mafanikio na imani ya kile alicho kuwa anakitamania na kukiamini kwa muda mrefu kama sehemu ya maisha yake (modeling)............................... Wakati anaanza safari yake ya matumaini katika kupigania ndoto zake ndani ya modeling alianza na neno "Ipo siku" na alivyo zidi kusogea mbele zaidi akasema tena "Nimefika lakini bado si sehemu nayo taka kuwa"....................................... Furaha yake na lengo lake kubwa ilikuwa ni siku moja kutambulika na kuheshimika  zaidi Africa na dunia kwa ujumla kama South Africa's First International Male Model with Albinism na kweli mpaka sasa furaha yake katika ndoto hizo imesha onekana nakuwa sehemu ya mfano wa kuigwa :

Tulio wengi katika kuishi maisha ya kufanikiwa ndani ya ndoto zetu tulizo jiwekea huwa tunashindwa kufanikiwa na kuonekana wenye kukataa tamaa kwa sababu ya kutokuwa na msimamo wa mawazo,nia,kujiamini,utayari,kuthubutu na kujitokeza............................................... Unacho takiwa kujua ni kwamba maamuzi ya nguvu za kufanikiwa katika kile unacho kiamini kama sehemu ya maisha yako "vipo juu yako"

No comments:

Post a Comment