Wednesday, October 12, 2016

SOMA HISTORIA YA CHE” GUEVARA MWANAMAPINDUZI HATARI DUNIANI,ALIYEONGOZA MAPINDUZI NCHINI CUBA

49 YEARS AFTER HIS ASSASSINATION:CELEBRATING LIFE & TIMES OF CHE GUEVARA

Jina lake halisi:Dr.ERNESTO RAFAEL GUEVARA de La Serna
Aliyefariki tarehe kama ya leo:9/10/1967

Mahali alipofia:La Higuera,Valle Grande-Bolivia.
Mzaliwa wa mji wa Rozario-Argentina,aliyepata masomo yake ya Udaktari katika chuo kikuu cha Bunos Airea(University of Bunos Aires)
Akiwa amezaliwa ktk familia yenye kipato cha kati,kwa leo tungemuita “mtoto wa kishua” CHE
Akiwa amebakiza mwaka mmoja kabla ya kumaliza masomo yake ya Udaktari,alitumia likizo kusafiri kwa pikipiki (Motorcycle) akiwa na rafikiye ALBERTO GRANADO na kutembea katika mataifa mbalimbali ya Amerika kusini ikiwemo Peru,Guatemala na akiwa katika,Safari alishuhudua Umasikini uliokithiri,Maradhi na unyonyaji wa jamii kutoka kwa makampuni ya kibwanyenye yaliyowekeza katika Amerika kusini.Akiwa Guatemala alishuhudia kupinduliwa kwa Rais Mzalendo,JACOB ALBERZ aliyechaguliwa na wananchi akiwa amelenga kurudisha Ardhi iliyokua imeporwa na Kampuni ya Kimarekani;AMERICAN FRUIT COMPANY.

Rais JACOB ALBERZ alipinduliwa kwa mpango wa CIA waliolenga kulinda maslahi ya Kampuni AMERICAN FRUIT COMPANY
Kwa mujibu wa yeye mwenyewe CHE GUEVARA katika Memoir yake,anasema alitamani baada ya kumaliza Masomo yake ya Udaktari ajikite hasa katika utafiti,awe mtafiti(Researcher)
Lakini kile alichokishuhudia GUATEMALA,PERU nk.kilitosha kubadili mawazo kuona kuna haja ya kuwa Mwananapinduzi kukomboa jamii kubwa aliyotopea ktk Umasikini na Unyonyaji
Baada ya kuhitimu masomo yake ya Udaktari aliondoka Argentina kuelekea Mexico alikokutana na RAUL CASTRO na FIDEL CASTRO wakiwa uhamishoni baada ya jaribio la kuvamia kambi ya jeshi ya Moncada na kumpindua Dikteta Fulgencio Batista kushindikana ikiwa ni mwaka 1957
Wakitumia Boat kwa jina “GRANMA” kutoka MEXICO walisafiri hadi CUBA walipoanza mapambano ya kumuondoa Dikteta Kibaraka wa marekani Fulgencio Batista,vita iliyodumu kwa miaka miwili mpaka mwaka mpya mwaka 1959 walipofanikiwa kuingia HAVANA wakitokea Milima ya Sierra Maestra,Santiago de CUBA. walikopigana vita ya msituni kwa miaka miwili kupitia vugu vugu la Julai 26(Julai 26 movement) lilioaisisiwa mwaka 1953 wakati wa jaribio la kuvamia na kupora silaha ktk kambi ya Jeshi ya Moncada kufeli.

Mwaka mpya 1959 yaani 1/1/1959 FIDEL,RAUL,CHE na CAMILO waliingia Havana na kuhitimisha mapinduzi,huku wakishangiliwa na maelfu ya wa CUBA waliojitokeza kuwalaki wapambanaji mahiri wakombozi wa CUBA huku Dikteta kibaraka Fulgencio Batista akikimbilia Marekani
Baada ya mapinduzi CHE alipewa majukumu makuu matatu:Waziri wa Viwanda,Mkuu wa Idara ya Ulinzi na Mkuu wa Benki kuu aliyesaini sarafu ya CUBA. “Peso” kwa jina lake “CHE”
Baada ya Mapinduzi FIDEL alimtuma CHE GUEVARA Katika mataifa mbali mbali kuimarisha Urafiki alikwenda Ulaya,Urusi,Asia na Afrika katika mataifa ya Algeria,Guinea,Misri nk.
Baada ya Safari hii aligundua bado kuna Mataifa mengi hayajapata Uhuru na Vita ya ukombozi inaendelea kuanzia Afrika,Asia na Amerika kusini pia.
Baada ya kukamilisha Ziara hii ndefu aliporejea HAVANA aliandika barua na kujiuzulu vyeo vyake vyote serikalini ikiwa ni pamoja na Uraia wa CUBA aliupata baada ya mapinduzi ya mwaja 1959.
Katika Barua ya kujiuzulu aliyomwandikia FIDEL alimweleza haoni sababu ya kuwa na vyeo serikalini wakati bado kuna watu wanateseka ktk mataifa mbalimbali,alimoumba FIDEL na serikali imtunzie Mkewe ALEIDA MARCH na Wanawe Ernesto,Aleida,Rafael maana inawezekana wanaweza wasimuone tena.Barua hii ilisomwa ba FIDEL ktk mkutano wa Hadhara jijini HAVANA waCUBA walilia na kusikitika juu ya maamuzi ya CHE
CHE alielekea ZAIRE(DRC) ya sasa akipitia Tanganyika(Tanzania) akivuka Ziwa Tanganyika na wapiganaji wake kadhaa aliotoka nao CUBA.Wakati huo LAURENT KABILA akiwa msituni anapigana kumuondoa Dikteta MOBUTU SE SEKO.CHE alikatishwa tamaa na udhaifu wa wapiganaji walioongozwa na Laurent Kabila walijikita kwenye Ulevi,ngono na Uporaji wa madini,CHE alirejea Tanganyika akikaa kwa muda na hatimaye kuelekea Bolivia ambapo wapiganaji walikua wakipigana na serikali Dhalimu.
Huku CIA wakimfuatilia wakimtumia kibaraka wao raia wa Cuba aliyekimbia marekani baada ya Mapinduzi FELIX RODRIGUEZ.ambaye alihibitisha uwepo wa CHE Bolivia
“CHE” alikamatwa na jeshi la Bolivia kwa maelekezo ya CIA akafungiwa katika nyumba moja iliyoko ktk eneo la Shule ktk kijiji cha LA HIGUERA-Mji wa Valle Grande baada ya mapigano makali na kupigwa risasi mguuni hivo kushindwa kukimbia hatimaye kukamatwa,ambapo FELIX RODRIGUEZ alituma telegraph Washington akajibiwa CHE GHEVARA auawe
Saa sita mchana tarehe 9/10/1967 kijana mdogo mwenye cheo cha Sajenti aitwaye:MARIO TERAN akiwa amelewa aliingia ktk Chumba alichokua amefungwa “CHE” na Bunduki
CHE GUEVARA alilomuona alimwambia “NAJUA UMEKUJA KUNIUA,NIPIGE RISASI WE MUOGA ILA UJUE UNAUA MWANAUME” English; “I KNOW YOU COME TO KILL ME,SHOOT COWARD BUT YOU ARE GOING TO KILL A MAN”
Habari za kuuawa CHE GUEVARA zilisambaa ulimwengu mzima kukawa na maombolezo na maandamano maeneo mbalimbali ulimwenguni kupinga Mauaji yake.Mwili wa CHE ulikatwa viganja kwa ajili ya CIA Kujiridhisha km ni CHE GUEVARA aliyeuawa kwa vipimo vya DNA.
CHE alizikwa katika kaburi la siri ambalo halikujulikana mpaka mwaka 2007 wataalamu(Archeologist) walipogundua kaburi lake huko Valle-Grande,Bolivia,Mabaki ya mwili wake yalipelekwa CUBA kwa Ndege maalum na kuhifadhiwa katika jengo la Makumbusho la CHE GUEVARA(CHE GUEVARA Museleom)-Jijini HAVANA
Mtoto pekee wa CHE GUEVARA ambaye yuko hai leo ni Dr.ALEIDA GUEVARA,Daktari bingwa wa watoto(Pediatrician) aliyeachwa na Baba akiwa na mwaka mmoja,ambaye serikali ya CUBA ilihudumia familia ya CHE baada ya kifo chake
Huyo ndo CHE GUEVARA kwa kifupi ambaye T-shirt zake zinavaliwa sana,Picha yake ni mashuhuri sana ktk stika za magari,na maeneo mbalimbali Ulimwenguni
Ceremos Como CHE,yaani “Tutakua kama CHE“ ni kauli mbiu ambayo watoto wadogo wa shule za msingi Nchini CUBA hufunzwa na kutumiwa km salam:CEREMOS COMO CHE
Long Live COMMANDANTE
Viva La Revolucion
HASTA LA VICTORIA SIEMPRE…!!! Until Victory Forever
Patria O Muerte,Vencermos ……… Homeland or Death,We shall Overcome
VIVA Commandante CHE GUEVARA

No comments:

Post a Comment