Thursday, February 11, 2016

MSAADA KWA KIJANA HUYU

TAARIFA KWA  WADAU.

Wadau wote wa TAS MOROGORO.naomba michango yenu ya kifedha ili kumsaidia ndugu yetu Omary ili aweze kwenda hospitari kutibiwa jicho lake.

Naomba kwayeyote atakaeguswa na jambo hili aweze kutoa alicho nacho ili kutimiza kiwango kinacho hitajika ambacho ni LAKI MOJA TU.

Tafadhari tuma mchango wako mojakwamoja kwa muhusika kwa namba yake 0713376426. Ningependa kwa muhusika ndugu omary wote watakao kuchangia tafadhali Taja humu ndani.

KUTOA NI MOYO, LEO KWAKE KESHO KWETU. Asanteni wenu katika ustawi wa watu wenye ualbino.

Hassan S Mikazi
Mwenyekiti TAS Mkoa wa Morogoro.


SARATANI YA MACHO KWA ALBINO

Kijana Omary hakiwa hospital Kenya kwa upasuaji wa macho kutokana na kuharibika kwa ushambuliwa na saratani.

Tunapenda kuwajulisha watanzania wote tunaitaji Masada kwa kusaidia kupunguza tatizo.

Karibu chamachaalbinomorogoro/ instagram tunapatikana.


SARATANI YA MACHO KWA ALBINO

Tatizo la saratani ya macho kwa alibino kwasasa ni tatizo kubwa huyu nimoja ya mgonjwa akiwa muhimbili hospital.

Bw.Yasini/ katibu wa@chamachaalbinomorogoro kwa michango tunaomba kupata huduma nzuri tunaomba msaada wenu.

Tufuate @chamachaalbinomorogoro


Monday, February 8, 2016

WATU 19 WAMEHUKUMIWA KIFO,BAADA YA KUKUTWA NA HATIA YA KUUA WALEMAVU WA NGOZI.

Watu 19 wamehukumiwa kifo baada ya kukutwa na hatia ya kuwaua walemavu wa ngozi (Albino).ni miongoni mwa watu 133 ambao walikamatwa kati ya mwaka 2006 hadi mwaka jana.

Hii ilikuja baada ya Bw.Masauni,kujibu swali kutoka kwa Mbunge wa viti maalumu Bi Mgeni Jadi Kadika (CUF) ambaye alitaka kufahamu Serikali inafanya nini kutokomeza mauaji ya Maalbino nchini.

Bw Masuani alisema Serikali imeongeza ulinzi kwaajili ya kuwalinda walemavu wa ngozi Nchini.

Alisema Serikali imeanda sehemu maalumu kwajili ya walemavu wa ngozi,na kuhakikisha wanaishi katika mazingira salama,na pia kuelimisha umma kuhusu mauaji ya kikatili dhidi ya Maalbino.

Tuesday, December 8, 2015

KIJANA KIONGOZI MWANAHARAKATI

Malila machim @malilerlovedejo apata dili ya kuwa mmoja wa wanachama na mwanaharakati wa watu wenye ulemavu wa ngozi au ualbino mkoa wa morogoro.

LEVEL ZA MVULANA BOYA NI

1. Kama umetembelewa na demu ile ameingia chumbani kwako tu mmekaa muda mara anakwambia funga mapazia na mlango alafu akawasha sabufa kwa sauti ya juu na wewe ukakaa kama zezeta unashangaa ka uko feri huo ni uboya na wewe una MSINGI mzuri wa uboya. 2 Kama upo na demu geto mnacheki movie alafu anakwambia yupo bored hainjoi hiyo movie unamwambia uweke nyingine anakataa unamuuliza anataka nini anakutizama machoni anatabasamu kidogo wewe huelewi ufanyaje unaenda kutafuta CD ya movie ya Rambo jua wewe ni boya level ya SECONDARY yaani hapo ni A ya uboya unasubiri kwenda Chuo 3. Upo na demu getto mmechili mnampigishana story za hapa na pale mara anakuambia kuna kitu anatakitamani kwa siku hiyo wewe huelewi hata tone ndio kwanza unakazana kumuonesha picha zako za shule ya msingi yeye anakwambia anataka kuondoka unaendelea kumuonesha sijui picha kwenye gallery yako na yeye kila mara anakuambia anataka kuondoka na wewe hujiongezi hujui anamaanisha nini basi jua wewe ni boya mimi nakutunuku CERTIFICATE ya UBOYA 4. Kama upo na demu getto kwako kwenye sofa mnapiga story na kucheki series ya Vampire Daries akakwambia uitoe uweke CD yeyote ile ambayo ni romantic ukamuwekea mkaangalia akawa anainjoi sana ghafla akatoka kwenye sofa na kujitupa kitandani alafu akakwambia mlale huku mkipiga story wewe ukaenda na kuanza kumsimulia hadithi za Sungura na Fisi Mara alifu lela uliwe basi umeshaufaulu mtihani wa Uboya na umepewa DEGREE yake

Sunday, October 4, 2015

TABIA YA WATU WASIO NA MAFANIKIO

1. Ni watu wenye tabia ya kujipendelea wao wenyewe, watu wenye umimi na ubinafsi wakati wote 2. Ni watu wenye tabia ya ubishi na kupinga kila jambo, hususani lile ambalo mwingine amelisema ama kulizungumza, kwao hoja ya mwingine sio hoja bali hoja yao ndiyo hoja pekee. 3. Ni watu wenye visasi na mafundo ya moyoni hata katika vitu vidogo na visivyo vya msingi, wanaweza kuzira kirahisi tena kwa muda mrefu bila hata sababu ya msingi 4. Wanaumizwa sana pale mwingine anapopewa pongezi au kusifiwa au kupewa ushindi, kiu yao ni kwamba pongezi zote na sifa zote na ushindi wote uwe wakwao. Mara mwingine anapoonekana kushinda basi wao hujifanya ndio waliokuwa chachu au wasababishaji wa ushindi huo na kwahivyo wanataka wapongezwe wao au mchango wao kukubalika mbele za watu 5. Ni watu walalamishi sana na wenye kulaumu kila mazingira, huwalaumu wengine pale wao wanapoonekana kushindwa, wakishindwa au kufeli wao basi huzitupia lawama kwa watu wanaowazunguka, utasikia wakisema “kama asingekuwa fulani basi nisingeshindwa hivi, yeye ndiyo amesababisha mimi kufeli au kutofanya vizuri” 6. Wanapenda na wala hawaoni tatizo kupoteza muda, anaweza kukaa mbele ya televisheni masaa na masaaa bila kujali muda unavyopotea 7. Mara nyingine hujaribu kujiwekea mpangilio wa siku wa nini atafanya na wakati gani lakini kamwe hawawezi kufwata walichokipanga wenyewe 8. Ni waoga na wapinzani wa mabadiliko hata kama hawanauhakika nini asili ya mabadiliko hayo 9. Mara zote hudhani na hufikiri kuwa wanajua kila kitu, ni ngumu sana kuishi na mtu wa aina hii kwa maana wakati wote ni ngumu kumbadili au kubadili lile analoliwaza au kulifikiri maana yeye anauhakika kuwa anafahamu kuliko mwingine yeyote 10. Katika kila wanalofanya wao husukumwa na mawazo au kiu ya kujua nini anafaidika nacho, kama yeye hapati manufaa ya moja kwa moja katika chochote afanyacho basi hawezi kushiriki chochote. Watu wahivi ni ngumu sana kusaidia mtu mwingine au kutoa mchango wa hali na mali kwa jamii maana wao huona kuwa hauna faida za moja kwa moja kwake. 11. Ni watu wanaopenda kuwazungumzia wengine, huzungumzia madhaifu ya watu na kushindwa kwa wengine, hata siku moja hawawezi kujadili mafanikio ya mtu mwingine 12. Mara nyingi ndani ya mioyo yao huwaza au kutamani wengine washindwe au wasiendelee, tena sio kutamani tu bali huumia wanapoona wengine wanafanikiwa 13. Sio wepesi wa kutoa taarifa muhimu kwa wengine, ni wafichaji wa taarifa za muhimu maana ndani yao wanakiu ya kuzuia maendeleo yaw engine au kuona wengine wanafanikiwa 14. Hawafahamu wala hawajui nini wanatamani wala ni nini wanataka maishani, kwa maana hiyo ni ngumu kufikia katika mustakabali wowote 15. Ni watu wenye hasira au kushindwa kujizuia kuonyesha hasira zao 16. Ni watu wasio na malengo, wasioweka malengo binafsi na wala hawawezi kuyafuata malengo yao, kwa hali hiyo basi inakuwa ngumu kufikia mafanikio maishani mwao.