Watu 19 wamehukumiwa kifo baada ya kukutwa na hatia ya kuwaua walemavu wa ngozi (Albino).ni miongoni mwa watu 133 ambao walikamatwa kati ya mwaka 2006 hadi mwaka jana.
Hii ilikuja baada ya Bw.Masauni,kujibu swali kutoka kwa Mbunge wa viti maalumu Bi Mgeni Jadi Kadika (CUF) ambaye alitaka kufahamu Serikali inafanya nini kutokomeza mauaji ya Maalbino nchini.
Bw Masuani alisema Serikali imeongeza ulinzi kwaajili ya kuwalinda walemavu wa ngozi Nchini.
Alisema Serikali imeanda sehemu maalumu kwajili ya walemavu wa ngozi,na kuhakikisha wanaishi katika mazingira salama,na pia kuelimisha umma kuhusu mauaji ya kikatili dhidi ya Maalbino.
No comments:
Post a Comment