Imewekwa Tarehe February 25, 2016
Ugonjwa wa Kansa wadaiwa kuwa changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino.
Ugonjwa wa Kansa wadaiwa kuwa changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino.
Watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) wanaoishi vijijini, wana hatari ya kupata magonjwa ya saratani ya ngozi, kutokana na kutokuwa na elimu ya afya bora na utunzaji wa ngozi.
Ugonjwa huo unatokana na ukosefu wa elimu ya utunzaji wa afya ya ngozi kwa walemavu waishio vijijini. Walemavu hao wana hatari kubwa ya kupatwa na saratani ya ngozi kutokana na ukosefu huo wa elimu, unatokana na umasikini.
Hata hivyo walemavu walio wengi, hawana elimu ya kutosha ya utunzaji wa afya zao, hali inayochangiwa na ukosefu wa kipato cha kuwasaidia katika kujikwamua na hali ngumu na ununuzi wa dawa hizo.
Katika hatua nyingine elimu ya afya, kwa kuangalia zaidi walemavu wanaoishi vijijini inahitajika nchini Tanzania . Vijijini ni sehemu ambayo kuna changamoto nyingi za maisha kuhusu namna ya kukabiliana na utunzaji bora wa afya zao.
No comments:
Post a Comment