Mwanamke mkongwe nchini Zimbabwe, wakati wa maandamano nje ya ukumbi wa baraza la jiji la Bulawayo.
Walikuwa wanaonesha kwamba hawana vyakula vya kutosha kutokana na kudorora kwa uchumi.
Picha/AFP, Getty #bbcswahili #Zimbabwe #mwanamke:
Mwanamke mkongwe nchini Zimbabwe, wakati wa maandamano nje ya ukumbi wa baraza la jiji la Bulawayo.
Walikuwa wanaonesha kwamba hawana vyakula vya kutosha kutokana na kudorora kwa uchumi.
Picha/AFP, Getty #bbcswahili #Zimbabwe #mwanamke:
Makumi ya maelfu ya wafuasi wa upinzani wamekusanyika mjini Kinshasa, Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, kupinga uwezekano kuwa uchaguzi wa rais huenda ukaahirishwa.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanywa Novemba, lakini tume ya uchaguzi, imesema inaweza kuchukua miezi 16, kurekibisha orodha za wapigaji kura.Upinzani unaona kuna jaribio la kuahirisha uchaguzi, ili kumruhusu rais Joseph Kabila abakie madarakani.
Kufuatana na katiba ya nchi hiyo kubwa ya Afrika , Rais Kabila anatakiwa kuondoka madarakani mwaka huu, baada ya kutumika kwa mihula miwili.Hata hivyo mahakama ya kikatiba nchini humo yameamua abakie madarakani, hadi uchaguzi utapofanywa.
#BBC:
Mhe Lembeli amerudi chama kubwa CCM hivi mchana wa leo katika mkutano mkubwa wa Mhe Mwenyekiti wa CCM na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli... Huko mjini Kahama. Anasema haoni sababu ya kwenda na "..safari ya uhakika isiyo na uhakika... kule hamna kitu."
Mafuriko mashariki mwa India na nchini Nepal yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 100 na kuwaathiri mamilioni ya wengine.
Mito iliyojaa maji imesababisha vijiji kufurika na kuwalazimu maelfu ya watu kuhama makwao.
Katika majimbo ya India ya Assam na Bihar, makundi ya uokoaji yanatumia mashua kuwafikia watu ambao wametafuta hifadhi katika makao ya muda kwenye sehemu zilizoinuka.
#BBC
Dar es Salaam. Siku moja baada ya Rais John Magufuli na Chadema kutoa misimamo tofauti kuhusu kupigwa marufuku kwa mikutano ya kisiasa, Jeshi la Polisi limemuita Freeman Mbowe kwa mahojiano, huku hafla ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili ambayo Edward Lowassa angekuwa mgeni rasmi ikizuiwa.
Katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji naye ameendelea kusisitiza msimamo wa chama chake wa kuitisha mikutano nchi nzima Septemba Mosi, kauli aliyoitoa saa chache baada ya Rais Magufuli kusisitiza msimamo wa kuzuia maandamano na mikutano ya kisiasa isipokuwa kwa wale walioshinda kwenye udiwani na ubunge ambao watatakiwa kufanya hivyo kwenye maeneo yao tu. #mwananchi
Jeshi la polisi mkoani Arusha, limewaita kwa mahojiano, mbunge wa Karatu,Wilbroad Qambalo, mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso na Mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu,Jubilate Mnyenye kutokana na kupuuza agizo la kutofanya mikutano ya hadhara katika jimbo hilo. Mwingine ambaye ametakiwa kwenda kuripoti polisi ni Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu, Lazaro Bajuta.
Wakizungumza jana baada ya kukabidhiwa barua za wito wa polisi, Qambalo na Paresso walisema wamestuka kutakiwa kuripoti ofisi ofisi ya Mkuu wa upelelezi mkoa wa Arusha jumatano.
Parreso alisema,walipokea barua jana saa sita mchana na kutakiwa kuripoti kwa RCO, saa nane lakini wakampigia na kumweleza wana ratiba nyingine tayari waende jumatano na akakubali.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkombo alipotakiwa kuelezea agizo hilo alisema yupo likizo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi.
Ametoa kauli hiyo leo asubuhi wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.
“Jana nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma ifikapo Septemba,” amesema Majaliwa na kushangiliwa na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma waliohudhuria maadhimisho hayo.
Amesema tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, kazi nyingi zimefanyika na wananchi wameziona na kwamba sasa hivi kazi iliyobakia ni utekelezaji wa ahadi alizotoa Rais John Magufuli.
“Wananchi kazi mmeziona na sasa tunaenda kwenye utekelezaji. Ninatoa agizo kuwa mawaziri na manaibu wote wahame mara moja kutoka Dar es Salaam na kuja Dodoma.
Wana ofisi ndogo Dodoma na kwa kuwa wamekuwa wakiishi wakati wote wa Bunge, wahamie mara moja. Mimi nahamia Septemba na utekelezaji wake nitausimamia kwa juhudi zote,” alisisitiza.
Amewataka wakazi wa Dodoma watumie fursa hiyo kutunza amani ya nchi na kudumisha umoja uliopo na pia akataka watumie fursa hiyo kujenga nyumba za kuishi za kutosha, nyumba za kulala wageni na hoteli za kitalii ili watu watumishi na wageni wanapokuja wasipate taabu mahali pa kuishi.
HUYU NDIO YULE ANAEVAA SUTI NA KUANGAIKIA AU KUELIMISHA KUHUSU ALIBINISIMU@suleimanmagoma
Moja ya sehemu zinazo nipa mkate wa kila siku. Am very grateful to this place and i love my job.. Karibuni HASHTAG SQUARE tunauza juice ya miwa iliyoandaliwa katika mazingira yanayozingatia Usafi. Utapata Juice ya Miwa pamoja na bites mbalimbali.
Tunapatikana stendi ya Makumbusho lango la kutokea Magari mkabala na mti wa mbuyu. Karibuni sana mniunge mkono.
Cku mojamoja mtu mzima nasimamia mpango mzima mwenyewe.Kuwa na maisha bora c jambo rahisi ni lazima Upige kazi kwelikweli na uwe mbunifu kila kukicha na kumuomba Allah.. wengi waliofanikiwa wametumia njia hizo. Nawashangaa sana baadhi ya watanzania wenzangu ambao hawataki kufanya kazi wanaamini eti Kiungo cha Mtu mwenye Albinism kina leta Utajiri. Tuwapuuze watu wenye fikra na mitazamo hiyo na Tuwape Elimu ya kutosha ili waelewe kuwa hamna shotcut katika maisha inabid wajitume katika kufanya kazi zilizo halali. #albinismawarenessfoundation
KARIBUNI sana HASHTAG SQUARE
Wakuu katika maeneo ya Kusini mwa Ujerumani, wamesema kuwa mtu mmoja amejilipua ndani ya baa na kuwajeruhi watu wengine 12, watatu kati yao vibaya sana.
Maafisa wa serikali wanasema mshukiwa ni raia wa Syria ambaye alikuwa ameshindwa kupata hifadhi nchini Ujerumani mwaka jana.Mlipuko huo ulitokea katika mji wa Ansbach karibu na tamasha moja la muziki ambalo ni maarufu sana katika eneo hilo.
Zaidi ya watu elfu mbili wameondolewa kutoka katika tamasha hilo, ambalo baadaye lilisitishwa.
Baadhi ya maeneo ya mji huo wa Ansbach, yamezingirwa na walinda usalama.Ni shambulio la tatu huko Bavaria, katika kipindi cha wiki moja.Ijumaa, watu tisa walifariki shambulio la ufyatuaji risasi mjini Munich na siku chache awali, kijana aliwashambulia watu kwa kisu na shoka kwenye treni.
#BBC
Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, amefuta uteuzi wa Naibu Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Hafidh Ussi Haji huku akimteua Khadija Shamte Mzee, kuchukua nafasi hiyo.
Pia, taarifa ya Ikulu inaonyesha Dk Shein, amemteua Amour Hamil Bakari kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar kuchukua nafasi ya Abdi Khamis Faki ambaye anastaafu kwa mujibu wa sheria.
Vilevile, Dk Shein amemteua Umi Aley kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Magazeti ya Serikali; Said Bakar Jecha na Sebtuu Mohammed Nassor wameteuliwa kuwa Makamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, wakati Ali Saleh Mwinyikai ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Zanzibar.
Wengine walioteuliwa ni Maryam Hamdan kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni, wakati Maryam Abdulla Yussuf ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani Zanzibar na Profesa Ali Seif Mshimba, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Zanzibar. Uteuzi huo unaanza Julai 25.
BAADA ya wiki jana kutangaza orodha ya vyuo ambavyo havitaruhusiwa kudahili Wanafunzi Kwa Mwaka wa Masomo 2016/17, leo Tume hiyo imetoa orodha nyingine ya vyuo ambavyo vimefungiwa kufanya udahili kutokana na sababu mbalimbali. Vyuo vilivyozuiwa kudahili ni pamoja na;
1. Katavi University of Agriculture - Kozi zote.
2. Ekernforde Tanga University - Kozi zote.
3. Hubert Kairuki Memorial University - Kozi ya udaktari.
4. Muslim University of Morogoro - Kozi ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma.
5. St. Joseph University In Tanzania (St.Mark's University College) - Kozi zote.
6. United African University of Tanzania - Kozi zote.
7. Tanzania International University - Kozi zote.
8. Kampala International University, Dar es Salaam College - Kozi ya Sayansi ya Kompyuta.
9. St. Joseph University College of Management and Commerce - Kozi zote.
10. Tumaini University, Dar es Salaam College - Kozi ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma.
12. Stefano Moshi Memorial University College - Kozi zote.
13. Teofilo Kisanji University, Tabora campus - Kozi zote.
14. University of Arusha, Musoma campus - Kozi zote.
15. Mount Meru University, Mwanza campus - Kozi zote.
16. University of Mbeya - Kozi zote.
17. Mzumbe University, Mwanza campus - Kozi zote.
18. Stella Maris Mtwara University College - Kozi zote.
19. ArchBishop James University College - Kozi zote.
20. Mwalimu Julius K. Nyerere University of Science and Technology - Kozi zote.
21. Josiah Kibira University College - Kozi zote.
22. College of Business Education, Mwanza campus - Kozi zote za shahada na shahada na Shahada ya Uzamili.
Kwa taarifa zaidi tembelea
http://www.tcu.go.tz
☝
Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Gilbert Simya na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga Robert Mageni waliosimama nyuma wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa chama cha albino wilaya ya Mbinga, baada ya kukabidhi msaada wa mafuta yenye thamani ya shilingi laki 8 yaliyotolewa na chama cha walemavu wilayani humo kwa ufadhili wa hospitali ya KCMC ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma Robert Mageni,akiteta jambo na mtoto mwenye ualbino ambaye hakufahamika jina lake mara moja wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mafuta maalum ya kuzuia magonjwa kwa watu wenye ulamavu wa ngozi yaliyotolewa na chama cha albino wilaya ya Mbinga.
Sista Judith Mwageni wa shirika la mtakatifu Wiliam jimbo la Mbinga akiwatambulisha watoto wenye ualbino wanaolelewa na kanisa katoriki jimbo la Mbinga wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa mafuta maalum ya kuzuia magonjwa ya ngozi yaliyotolewa na chama cha walemavu wilaya ya Mbinga.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga Robert Magenj akizungumza jana katika hafla ya kukabidhi mafuta maalum kwa watu wenye ualbino yaliyotolewa na chama cha walemavu wilaya ya Mbinga kwa ufadhili wa hospitali ya KCMC ya Moshi,katikati ni katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Gilbert Simya.
Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Gilbert Simya akitoa mafuta maalum ya kuzuia magonjwa kwa watu wenye ualbino jana wakati wa kukabidhi msaada wa mafuta wenye thamani ya shlingi laki 8 yaliyotolewa na chama cha walemavu wilayani humo.Picha na Muhidin Amri.
*Zuberi* alimpa ujauzito mwanafunzi
akashtakiwa.
Kumbe Zuberi ana bibi
yake mtaalamu wa yale mambo yao
ya Sumbawanga, akampachika Zuberi
jinsia ya kike alipofika mahakamani
kuhojiwa Zuberi akasema sijampa ujauzito kwani mimi nina jinsia ya kike.
Kwa kuthibitisha Zuberi akajifunua
nguo basi akashinda kesi, kufika
nyumbani Zuberi akawakuta watu
wamejaa wanalia, akauliza kulikoni?
Akaambiwa bibi yako amefariki.
Zuberi akawa *zubeda*
Mfanyakazi mmoja ametumbukia kwenye mtambo wa kusagia kokoto kwa bahati mbaya. Nandio ukawa mwisho wake wa kuishi. Imetokea huku mbeya