Wednesday, October 12, 2016

SOMA HISTORIA YA CHE” GUEVARA MWANAMAPINDUZI HATARI DUNIANI,ALIYEONGOZA MAPINDUZI NCHINI CUBA

49 YEARS AFTER HIS ASSASSINATION:CELEBRATING LIFE & TIMES OF CHE GUEVARA

Jina lake halisi:Dr.ERNESTO RAFAEL GUEVARA de La Serna
Aliyefariki tarehe kama ya leo:9/10/1967

Mahali alipofia:La Higuera,Valle Grande-Bolivia.
Mzaliwa wa mji wa Rozario-Argentina,aliyepata masomo yake ya Udaktari katika chuo kikuu cha Bunos Airea(University of Bunos Aires)
Akiwa amezaliwa ktk familia yenye kipato cha kati,kwa leo tungemuita “mtoto wa kishua” CHE
Akiwa amebakiza mwaka mmoja kabla ya kumaliza masomo yake ya Udaktari,alitumia likizo kusafiri kwa pikipiki (Motorcycle) akiwa na rafikiye ALBERTO GRANADO na kutembea katika mataifa mbalimbali ya Amerika kusini ikiwemo Peru,Guatemala na akiwa katika,Safari alishuhudua Umasikini uliokithiri,Maradhi na unyonyaji wa jamii kutoka kwa makampuni ya kibwanyenye yaliyowekeza katika Amerika kusini.Akiwa Guatemala alishuhudia kupinduliwa kwa Rais Mzalendo,JACOB ALBERZ aliyechaguliwa na wananchi akiwa amelenga kurudisha Ardhi iliyokua imeporwa na Kampuni ya Kimarekani;AMERICAN FRUIT COMPANY.

Rais JACOB ALBERZ alipinduliwa kwa mpango wa CIA waliolenga kulinda maslahi ya Kampuni AMERICAN FRUIT COMPANY
Kwa mujibu wa yeye mwenyewe CHE GUEVARA katika Memoir yake,anasema alitamani baada ya kumaliza Masomo yake ya Udaktari ajikite hasa katika utafiti,awe mtafiti(Researcher)
Lakini kile alichokishuhudia GUATEMALA,PERU nk.kilitosha kubadili mawazo kuona kuna haja ya kuwa Mwananapinduzi kukomboa jamii kubwa aliyotopea ktk Umasikini na Unyonyaji
Baada ya kuhitimu masomo yake ya Udaktari aliondoka Argentina kuelekea Mexico alikokutana na RAUL CASTRO na FIDEL CASTRO wakiwa uhamishoni baada ya jaribio la kuvamia kambi ya jeshi ya Moncada na kumpindua Dikteta Fulgencio Batista kushindikana ikiwa ni mwaka 1957
Wakitumia Boat kwa jina “GRANMA” kutoka MEXICO walisafiri hadi CUBA walipoanza mapambano ya kumuondoa Dikteta Kibaraka wa marekani Fulgencio Batista,vita iliyodumu kwa miaka miwili mpaka mwaka mpya mwaka 1959 walipofanikiwa kuingia HAVANA wakitokea Milima ya Sierra Maestra,Santiago de CUBA. walikopigana vita ya msituni kwa miaka miwili kupitia vugu vugu la Julai 26(Julai 26 movement) lilioaisisiwa mwaka 1953 wakati wa jaribio la kuvamia na kupora silaha ktk kambi ya Jeshi ya Moncada kufeli.

Mwaka mpya 1959 yaani 1/1/1959 FIDEL,RAUL,CHE na CAMILO waliingia Havana na kuhitimisha mapinduzi,huku wakishangiliwa na maelfu ya wa CUBA waliojitokeza kuwalaki wapambanaji mahiri wakombozi wa CUBA huku Dikteta kibaraka Fulgencio Batista akikimbilia Marekani
Baada ya mapinduzi CHE alipewa majukumu makuu matatu:Waziri wa Viwanda,Mkuu wa Idara ya Ulinzi na Mkuu wa Benki kuu aliyesaini sarafu ya CUBA. “Peso” kwa jina lake “CHE”
Baada ya Mapinduzi FIDEL alimtuma CHE GUEVARA Katika mataifa mbali mbali kuimarisha Urafiki alikwenda Ulaya,Urusi,Asia na Afrika katika mataifa ya Algeria,Guinea,Misri nk.
Baada ya Safari hii aligundua bado kuna Mataifa mengi hayajapata Uhuru na Vita ya ukombozi inaendelea kuanzia Afrika,Asia na Amerika kusini pia.
Baada ya kukamilisha Ziara hii ndefu aliporejea HAVANA aliandika barua na kujiuzulu vyeo vyake vyote serikalini ikiwa ni pamoja na Uraia wa CUBA aliupata baada ya mapinduzi ya mwaja 1959.
Katika Barua ya kujiuzulu aliyomwandikia FIDEL alimweleza haoni sababu ya kuwa na vyeo serikalini wakati bado kuna watu wanateseka ktk mataifa mbalimbali,alimoumba FIDEL na serikali imtunzie Mkewe ALEIDA MARCH na Wanawe Ernesto,Aleida,Rafael maana inawezekana wanaweza wasimuone tena.Barua hii ilisomwa ba FIDEL ktk mkutano wa Hadhara jijini HAVANA waCUBA walilia na kusikitika juu ya maamuzi ya CHE
CHE alielekea ZAIRE(DRC) ya sasa akipitia Tanganyika(Tanzania) akivuka Ziwa Tanganyika na wapiganaji wake kadhaa aliotoka nao CUBA.Wakati huo LAURENT KABILA akiwa msituni anapigana kumuondoa Dikteta MOBUTU SE SEKO.CHE alikatishwa tamaa na udhaifu wa wapiganaji walioongozwa na Laurent Kabila walijikita kwenye Ulevi,ngono na Uporaji wa madini,CHE alirejea Tanganyika akikaa kwa muda na hatimaye kuelekea Bolivia ambapo wapiganaji walikua wakipigana na serikali Dhalimu.
Huku CIA wakimfuatilia wakimtumia kibaraka wao raia wa Cuba aliyekimbia marekani baada ya Mapinduzi FELIX RODRIGUEZ.ambaye alihibitisha uwepo wa CHE Bolivia
“CHE” alikamatwa na jeshi la Bolivia kwa maelekezo ya CIA akafungiwa katika nyumba moja iliyoko ktk eneo la Shule ktk kijiji cha LA HIGUERA-Mji wa Valle Grande baada ya mapigano makali na kupigwa risasi mguuni hivo kushindwa kukimbia hatimaye kukamatwa,ambapo FELIX RODRIGUEZ alituma telegraph Washington akajibiwa CHE GHEVARA auawe
Saa sita mchana tarehe 9/10/1967 kijana mdogo mwenye cheo cha Sajenti aitwaye:MARIO TERAN akiwa amelewa aliingia ktk Chumba alichokua amefungwa “CHE” na Bunduki
CHE GUEVARA alilomuona alimwambia “NAJUA UMEKUJA KUNIUA,NIPIGE RISASI WE MUOGA ILA UJUE UNAUA MWANAUME” English; “I KNOW YOU COME TO KILL ME,SHOOT COWARD BUT YOU ARE GOING TO KILL A MAN”
Habari za kuuawa CHE GUEVARA zilisambaa ulimwengu mzima kukawa na maombolezo na maandamano maeneo mbalimbali ulimwenguni kupinga Mauaji yake.Mwili wa CHE ulikatwa viganja kwa ajili ya CIA Kujiridhisha km ni CHE GUEVARA aliyeuawa kwa vipimo vya DNA.
CHE alizikwa katika kaburi la siri ambalo halikujulikana mpaka mwaka 2007 wataalamu(Archeologist) walipogundua kaburi lake huko Valle-Grande,Bolivia,Mabaki ya mwili wake yalipelekwa CUBA kwa Ndege maalum na kuhifadhiwa katika jengo la Makumbusho la CHE GUEVARA(CHE GUEVARA Museleom)-Jijini HAVANA
Mtoto pekee wa CHE GUEVARA ambaye yuko hai leo ni Dr.ALEIDA GUEVARA,Daktari bingwa wa watoto(Pediatrician) aliyeachwa na Baba akiwa na mwaka mmoja,ambaye serikali ya CUBA ilihudumia familia ya CHE baada ya kifo chake
Huyo ndo CHE GUEVARA kwa kifupi ambaye T-shirt zake zinavaliwa sana,Picha yake ni mashuhuri sana ktk stika za magari,na maeneo mbalimbali Ulimwenguni
Ceremos Como CHE,yaani “Tutakua kama CHE“ ni kauli mbiu ambayo watoto wadogo wa shule za msingi Nchini CUBA hufunzwa na kutumiwa km salam:CEREMOS COMO CHE
Long Live COMMANDANTE
Viva La Revolucion
HASTA LA VICTORIA SIEMPRE…!!! Until Victory Forever
Patria O Muerte,Vencermos ……… Homeland or Death,We shall Overcome
VIVA Commandante CHE GUEVARA

Monday, October 3, 2016

True star Rukia

This is #truestar Rukia, the oldest resident of #Kabangacentre. Like many older persons, she has special needs. Even more so because she was born with albinism. 

At 58 she has not been able to shine her light onto the world .

For #international #day of #olderpersons we want to enohasize that, PWAs, whether children or full-grown adults, have the right to be themselves and live in freedom in their communities or wherever they choose to be!

From one of albinism society foundation found at kigoma @kabangastars  - letthemshine #kabangastars #kabanga #kigoma #kasulu #kabangacenter #beautifulplace #beautifulpeople #pwa #albinismawareness #internationalolderpersonsday #ngo #socialprojects #takeaction #inmyskiniwin #happymonday

Tuesday, September 20, 2016

Fund for Daniel

@Regrann from @realjaype  -  @Regrann from @iamtjan -  Pls lets not forget to donate something for Daniel.. It's not a project! It's a cause that is personal to his family and myself and also everyone... Daniel is currently on a potential donor list in India and we can do more and do better guys ! ��  I understand the importance of giving so much cos I have known what it felt like to want something and not have it... You can fund Daniel here https://www.gofundme.com/29ume2ng  Or Donate to #GiveDanielAHeart FCMB - USUANLELE DANIEL OSAYANDE FCMB 3469556012  #GiveDanielAHeart Your Prayers and Donations Go a long way Dear Nigerian.  #TeamDaniel #Regrann - #regrann 

Tuesday, September 6, 2016

TANGAZA HAPA BUREEEE

Je umewahi kufikiri kabisa wapo vijana kwa ajili ya kusaidiana basi karibu katika tovuti hii.

Hipo kwa ajili ya vijana wote kujitangaza kwa kazi zao buree,pengine hata pasipo kujuwa mtu husika.

Umenielewa sasa wewe jitangaze popote kwani ndio muda wako.

KUTANA NA MALILA AU MALILERLOVEDEJO ANAE JIKUBALI KULIKO UNAVYO FIKIRI

Marafiki ndio chanzo pengine tukashindwa kuaminiana..

Unaweza ukawaamini kufanya nao kazi waka kudondosha..

Kutana na malila machim peter au @Malilerlovedejo kijana mwanaharakati na mfanyaji wa kazi za sanaa pia ni mwanamitindo.

Niliamini rafiki zangu kupitia walivyo kuwa navyo yani ujuzi kufanya nao kazi nao na waka mdondosha.

Alitaka blog yake tu itengenezwe iwe nzuri tu.. akahamua ampe dili rafiki yake bado still akuweza kumtimizia ndoto yake ikiwa ni rafiki wapili kumpatia iliaweze kusaidia pia kutangaza, vipaji vya vijana na rafiki zake.

Achana na izo tu kwa uchache hata biashara alizo fanya na marafiki zake na kuhamini pia walimdondosha..

Amebaki na ndoto na Harakati zake mwenyewe na hakiamini katika yeye mwenyewe. kuwatangaza bila gharama yeyote na kuwa na imani kwa vijana wenzake wanaweza.

Kijana huyu anasema anajiamini yeye tu.. katika kutengeneza mtazamo chanya kupitia mitandao ya kijamii na anaona matunda yake.

Huyo ndio malila machim au muhite Lovedejo.. "anasema kidogo kibaya ..kutokujua pia ni nyenzo ya mafanikio.na jikubali Mimi tu.

Friday, August 5, 2016

LISSU AFIKISHWA TENA MAHAKAMANI

Dar es Salaam. Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu amefikisha Mahakamani  ya Kisutu saa  8. 46  huku mahakamani hapo kukiwa na ulinzi mkali.

Ulinzi umeimarishwa katika mahakamani hapo muda mrefu wakati wakimsubiria Lissu akitokea katika kituo cha polisi kanda maalumu.

Polisi wapatao tisa baadhi ya wakiwa na silaha  wametanda katika eneo la mbele la mahakama hiyo.

HOMA YA MANJANO: WHO LAWAMANI


Uchunguzi wa shirika la habari la AP umebaini kwamba shirika la afya duniani WHO lilitekeleza makosa makubwa katika kukabiliana na mlipuko wa homa ya manjano Afrika ya Kati.

Uchunguzi huo unasema chanjo milioni moja zilizokuwa zikisafirishwa hadi Angola zilitoweka kutoka kwenye shehena ya chanjo milioni sita za homa hiyo ya manjano.

Baadhi ya chanjo zilipelekwa katika maeneo ambayo hayakuwa yameathiriwa na homa hiyo, huku zilizopelekwa katika maeneo yaliyoathiriwa, zikikosa sindano.

#BBC