Thursday, May 26, 2016

TAS MOROGORO INATOA PONGEZI KWA WAZAZI, WENYE WATOTO WALIO NA HALI YA ALIBINO.

Kuhusu utunzaji bora wa mtoto mwenye ualbino nimuhimu sana mfano mzuri ni dadaetu Hawa Hassan tulimpatia Elimu ya ufahamu kusu malezi bora ya mtoto wake Wema.

Na leo mtoto huyu amekuwa kivutio kwakila mtu jinsi muonekano wa mtoto Wema anavyo onekana.

Hongera sana mama Wema na wazazi wengine kwa kutusikiliza ushauri wetu ambao umepelekea Wema Kuwa na afya bora ya ngozi.

Alisema mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualibino mkoa wa morogoro Bw.Hassan mikazi.

KANSA KWA WATU WENYE UALIBINO INAWEZEKANA

Kama wazazi na walezi watapatiwa Elimu ya kumtunza mtoto mwenye ualbino tatizo la saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino litapungua sana.

Nimuda muafaka sasa kwa wadau na serikali kutoa kuwapatia sunscreen lotion kwakila mtu mwenye ualbino ili kupunguza saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino hususan watoto.

Mkoa wa Morogoro unakadiriwa kuwa na watu wenye ualbino zaidi ya 15,000 wengiwao wanaishi vijijini na hawapatiwi vifaa tiba wala vifaakinga kama sunscreen lotion hali inayopelekea kuasirika na tatizo la saratani ya ngozi

BREAKING NEWZZ...

DIAMOND ÑA ALIKIBA WAPIGANA STUDIO

Wakiwa ndani ya studio ya Burn Records inayomilikiwa na 'chalii' Shedy Clever usiku msanii Diamond na hasimu wake mkubwa katika gemu la Bongofleva Alikiba..kulitokea mabishano makali kati ya wasanii hao hali iliyomnyima moyo wa subira Diamond na kujikuta akimrushia ngumi msanii mwenzake Alikiba...

Muda mchache uliopita inasemekana kwamba producer Shedy Clever aliwapigià simu wasanii hao akiwataka waende studio kwake kwa ajili ya kuwasikilizisha 'beats' alizoziandaa kwa ajili yao...
Katika hali ambayo kila mmoja hakutegemea kumkuta mwenzake studio hapo ilimpa wakati mgumu producer shedy baada ya wasanii hao kujikuta wakivutiwa na beat moja na kila mmoja alihitaji kulichukua kwa ajili ya kulitumia...
Wakati wakiendelea kugombea beat hilo walijikuta wakirushiana ngumi hali iliyopelekea kuvunjika kwa Computer ya studio humo...
Baada ya ugomvi kuwa mkali Shedy clever aliamua kupiga simu polisi na baada ya polisi kufika waliwakamata wasanii hao na kuwapeleka kituoni kwa mahojiano zaidi.....
                *     *      *
*JAMANIEEE NIKO FIELD NAJIFUNZA KUANDIKA HABARI ZA UDAKU......"*

Tuesday, May 24, 2016

ULIKUWA UJUI CHUKUWA HIYO

  ����������������������������������������
1. Kama upo SINGLE na umekazana kusema "SIAMINI MTU KATIKA MAPENZI" kumbuka rafiki zako wanaoa na kuolewa kila siku. Acha mawazo hasi omba Mungu akujalie mwenza wa maisha ambae unaendana nae.

2. Kama upo ndani ya ndoa na umekazana kusema "NAICHUKIA HII NDOA" huoni wanandoa wengine ambao wanasheherekea jubilei ya miaka 20 ya ndoa zao?  Omba Mungu aiponye ndoa yako.

3. Kama umekazana kusema "NAMWACHA MUME WANGU, KWANI ANANISALITI" tafadhali hebu nenda mjini pita maeneo ya Kona Bar, Kimboka na maeneo kama hayo uone wanawake malaya wenye uchu ambao wanamsubiri kwa hamu mumeo wamchune vizuri ambao kwao hawajali haya ku share mwanaume. Omba Mungu aitengeneze ndoa yako.

4. Usikazane kusema "NAICHUKIA KAZI YANGU" angalia maelfu ya vijana ambao hawana ajira wanazunguka kila siku na mabahasha maofisini! Vipi unataka kujiunga nao? Kuwa na shukrani!

5. Umekazana kusema unapachukia unapoishi, tafadhali sana nenda kawatembelee watoto wa mitaani uone mazingira magumu wanayoishi! Mshukuru Mungu walau unalala hata kwenye godoro.

6. Wengine husema "NIMECHOKA NA HAYA MAISHA" sawa nenda mahospitalini na uone watu wanavyopigania maisha yao, nenda mochwari na utizame na uniambie unafikiri nini! Cha Mihimu ni kushukuru Mungu

HEBU NISIKILIZE KWA MAKINI..... Kutambua thamani ya miaka minne au mitatu, muulize mhitimu wa chuo kikuu

Kutambua thamani ya mwaka mmoja, muulize mwanafunzi aliyefeli mtihani wake wa mwisho, kutambua umuhimu wa miezi tisa muulize mama aliejifungua mtoto aliye njiti!

Kutambua thamani ya wiki moja muulize mhariri wa gazeti linalotoka kila wiki.

Kutambua thamani ya dakika moja muulize abiria aliyechelewa safari ya ndege, basi au treni.

Na kutambua thamani ya sekunde muulize mtu yeyote aliyenusurika katika ajali!

Furahia kila dakika ambayo mwenyezi Mungu amekupa kuendelea kuvuta pumzi yake! Acha kulalamika maisha ni jinsi wewe unavyoishi!

Kama upo hai mpaka leo shukuru kwa kusema "ASANTE MUNGU"

Share it with your friend

Monday, May 23, 2016

KASHIFA YA CHINA NA NYAMA ZA BINADAMU WAFU

CHINA YAKANA KUUZA NYAMA YA BINADAMU AFRIKA
Wizara ya maswala ya kigeni nchini China imekana ripoti kwamba kampuni za chakula nchini humo zinaweka nyama ya binaadamu na kuuza barani Afrika kama nyama ya ng'ombe.

Chombo cha habari nchini humo Xhinua kimesema kuwa jarida moja nchini Zambia lilimnukuu kimakosa mwanamke mmoja ambaye hakutajwa anayeishi China.

Alisema kuwa kampuni za China zilikuwa zikichukua miili ya wafu kuitia katika viungo na kuiweka katika mikebe.

Msemaji wa China Hong Lei amesema kuwa ripoti hizo hazina uwajibikaji.

Balozi wa China nchini Zambia,Yang Youming ,amesema kuwa ripoti hizo zililenga kuharibu uhusiano mzuri kati ya mataifa hayo mawili. ''Leo jarida moja linasambaza uvumi ,likidai China inatumia nyama ya binaadamu ambayo uihifadhi katika mikebe na kuiuza Afrika. ''Hii ni dhulma ya makusudi ambayo haiwezi kukubalika kabisa kwetu sisi''.
#BBC

WANAWAKE NI TATIZO HILI

WANAUME TUSHIRIKI KATIKA SALA HII YA KUWAOMBEA WANAWAKE ...

1. Atakua na simu yake mpo nyumbani dakika hiyo anakwambia umbip hajui kaiweka wapi.
- Tuhurumie Baba

2. Ana Nguo zimejaa makabati mawili lakini hajui avae nini ukimwambia mtoke!
- Baba, ni magumu kwetu mambo haya.

3. Anakasirika ukikosa kumtumia text ya good night lakini yeye akikosa wewe inabidi uwe muelewa!
- Tuwaeleweje, Baba?

4. Ana viatu zaidi ya pea 50 lakini hana viatu vya kuvaa vya kwenda ibadani.
- Mungu uwasamehe

5. Akianza kuvaa saa moja atamaliza saa tano muda wote inabidi umsubiri tu.
- Si kupenda kwao Baba ila nasi yanatushinda Bwana

6. Akienda saloon anakaa kuanzia asubuhi mpaka jioni na huna budi kumsubiri na usilalamike.
- Mungu wetu, tupe moyo wa kuyahimili haya

7. Ana mafuta tofauti ya kujipaka mikono, shingo, kisogo, miguu, mpaka kisigino! Hata Mdomoni
- Ee Mungu ni Wewe uyajuaye mateso tuyapitiayo Baba

8. Mnaachana asubuhi akiwa na furaha, na ukirudi jioni amenuna hataki hata kukusalamia na ukiuliza tu balaa.
- Tupe uvumilivu ee Bwana!

9. Anajaribu ku match nguo na hereni na akiona hazifanani abadili nguo sababu tu ya hereni.
- Teremka uwashike mikono yao baba..

10. Mkitembea barabarani inabidi ukae upande wa barabara eti wewe ni mwanaume ukigongwa na gari haina noma.
- Eeh baba tuepushe na Hiki kikombe ulisema hawa ni wasaidizi wetu lakini tumekuja kuwa wafanyakazi wao.

Amen!!!!!!!!!!

JIFUNZE EWE MWANAMKE


1. Usikimbilie kuhama na kuondoka nyumbani kwa wazazi wako kabla hujajipanga vizuri.

2. Usimsubiri mwanaume ndio uanze maisha, unaweza ukaishi maisha yako mwenyewe na ukaweka msingi mzuri utakaokusaidia huko baadae.

3. Kaa mbali na marafiki waovu, jifunze kuheshimu kila mtu kuwa na busara na vaa mavazi ya heshima.

4. Usimchekee chekee kila mwanaume, kwa maana wengine sio waoaji ni chui waliojivika ngozi ya kondoo! Ni bora ukaendelea kuabki single kuliko uje kuolewa na mtu ambaye atakufanya ujute maisha yako yote hapa duniani. Omba Mungu akupe busara na ustahimilivu.

5. Jijengee tabia ya kula kwa afya, siku zote jitahidi ule milo yote mitatu acha kula biscuit na soda, usipendelee chips na mishkaki na vyakula vya aina hiyo. Fanya mazoezi mepesi kuuweka mwili wako uendelee kuwa mzuri wa kuvutia. Wewe ni tunu kwa mume wako mtarajiwa au uliyenae.

6. Vaa kwa heshima, watu watakujaji kulingana na jinsi tu ulovyovaa hata maongezi yao yataegemea kutokana na uvaaji wako.

7. Usitumie SEX kama njia ya kujihakikishia Mapenzi. Kufanya mapenzi sio tiketi ya kupendwa. Ata SEX na wewe na atakuacha kwenye mataa ya ubungo junction.

8. Usiolewe nae kwa vile ana pesa za kutosha na ni tajiri kwa sababu karibuni tu na wewe utakua moja ya mali anazomiliki.

8. Jiongezee thamani, get a career! Usiwe mpumbavu kufikiri mwanaume ndio atasuluhisha matatizo yako yote. Jibidiishe kwa kazi zako binafsi hakuna raha juu ya kuwa na maamuzi ya kutumia kile kipato ulichokipata kwa jasho lako.

10. Wewe ni wa muhimu mno, una thamani kubwa sana! Jipende jiheshimu, jijali. Usijali umetendwa na wangapi katika mahusiano! Usikate tamaa jiweke vizuri. Ishi maisha yako. Hayo unayopitia ni funzo tu ktk maisha.

Above all, Remember this, Charm is deceitful, and beauty is vain: but a woman that fears the LORD, she shall be respected.

MUNGU AWABARIKI WANAWAKE WOTE ULIMWENGUNI, ABARIKI KAZI ZA MIKONO YENU NA SIO KAZI ZA MAUNGO YENU. NINYI NI WA THAMANI MNO.