Thursday, October 28, 2010
http://www.bongostarlink.com/2010/10/mrisho-mpoto-asherehekea-siku-yake-ya.html
Jana majira ya mchana msanii mwenye kipaji cha pekee Mrisho Mpoto alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na watoto yatima wa pale CHAKUWAMA maeneo ya Sinza.
Mpoto nia ya kufanya hivyo ni kutokana mwaka huu 2010 ndani ya miezi 6 ameondokewa na ndugu zake watatu akiwemo Baba yake mzazi, Mama yake mzazi pamoja na mdogo wake wa kike ambao walikuwa wawili tu. Mpoto kwa kuwa aliona yuko peke yake sasa basi haina budi siku hii akasherehekee na watoto yatima kwa kupeleka viroba vya mchele na unga wa ugali pamoja na mafuta ya kupikia na kununua vinywaji na kunywa nao pale.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment