Wednesday, November 9, 2016

UTAFITI: MIKOPO YA WANAWAKE HUTUMIWA NA WANAUME ZAO KWENYE ANASA.


Matokeo ya utafiti wa kuangalia changamoto za ufanyaji biashara kwa mwanamke Tanzania umebaini kuwa wanaume hutumia mikopo ya wake zao kwa matumizi mingine ikiwamo anasa na pombe.Utafiti huo uliofanyika kati ya Julai 30 na Agosti 12 mwaka huu, umetolewa jana mbele ya wajasirimali wanawake nchini kupitia mkutano wa Chemba ya Wanawake wajasiriamali nchini.Utafiti huo ulihoji wanawake 154,makundi tisa na maofisa wa taasisi zisizo za kiserikali katika kanda sita za Tanzania bara.

 Mtafiti na mwasilishaji wa utafiti huo ,uliojikita kuchambua na kutoa mapendekezo ya kumwezesha mwanamke,Ndasile Chamkunde amesema zinahitajika juhudi ili kumsaidia mwanamke kuongeza uwezo wake kibiashara.

"Changamoto nyingine ni mchakato mgumu wa kusajili biashara zao, nusu ya waliohojiwa ndio  wamejisajili.” amesemaAmesema asilimia 75 wanauza katika soko la Afrika Mashariki ila asilimia 78 wanauza kwa muda tu, elimu yao ni chini ya kidato cha nne, na asilimia 48 wanategemewa na watu sita kupitia biashara zao, "amesema Chamkunde ambaye pia ni muhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha UDSM.
#Mwananchi

Monday, November 7, 2016

TANESCO YAOMBA KUONGEZA BEI YA UMEME MWAKANI


Dar es Salaam. Mchakato wa kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya ombi la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) la kuongeza bei ya nishati hiyo kwa wastani wa asilimia zaidi ya 18.9 ifikapo mwaka 2017, unatarajia kuanza.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imeeleza kuwa Oktoba 4, mamlaka hiyo ilipokea ombi la mabadiliko ya bei ya umeme, hivyo unaandaliwa mkakati wa kukusanya maoni ya wadau wa nishati hiyo.

“Mikutano ya ukusanyaji maoni kuhusu bei inayopendekezwa na Tanesco itaanza Novemba 16 katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha, Dodoma  na kwa Dar es Salaam ni Novemba 23,” inaeleza taarifa hiyo.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni miezi saba tangu kutangazwa kwa bei mpya ya umeme iliyokuwa na punguzo la asilimia 1.5 hadi 2.4 sanjali na kuondoa tozo ya kuunganishiwa umeme ya Sh5,000 na gharama ya huduma kwa kila mwezi ambayo ilikuwa na Sh5,520.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema shirika hilo limefanya tathmini na kujiridhisha kuwa hakuna hasara itakayopatikana endapo bei hiyo itatumika.  #mwananchi

MKUU WA WILAYA HAKABIDHI TV (RUNINGA)GEREZA LA TUNDURU

Mkuu wa wilaya ya Tunduru mh Juma Zuberi Homera ametimiza ahadi yake aliyotoa mara baada ya kuteuliwa na kulitembelea gereza la Tunduru kuwa atawapa wafungwa Runinga(TV) ili waweze kuona habari mbalimbali kwani ni haki yao kikatiba

Na TV yenyewe ndio hiyo hapo kama inavyo onekana katika picha

Friday, November 4, 2016

SEPETU NA MUNA KUVUANA NGUO

Maneno ya wemasepetu -  Rose Alphonce Nungu... Nakuita tena kwa mara ya pili Rose Alphonce Nungu.... Unanitafutia nini wewe mwanamke...!?

Nini nimekukosea wewe dada...? Niliapa na Miungu yote siwezi kupost kitu chochote kwa account yangu kinachokuhusu wewe ila wallahy wewe dada You are pushing my buttons...

Tena una push buttons zangu kikweli kweli cuz nimekaa kimya na yako mengi.... Usijisahaulishe leo nimekuja kwako na ukalia mno kutaka vitu visitoke kwenye mitandao...

Sasa nakwambiaje Rose, mimi sitovitoa mitandaoni cuz im nat dat illiterate kama wewe... But nataka kukuuliza kitu, kwanini unamfanya mama angu kama ndondocha wako...?

Let me tell u one thing, Rose, I have been in the industry kwa miaka 10, Never have I taken my mum kwenye sehemu za starehe tena usiku wa manane... Ntamuita mama angu pale ninapojua kuwa uwepo wa mam unahitajika kwenye hafla hii... Umekuja ukaamua kujiweka karibu na mama angu kiasi cha kwamba mimi tena nikawa sio shoga ako bali mama angu ndo ukamtawala.... Ulikuwa una yako...

Leo hii umeweza kumteka mama angu kiasi cha kwamba unamfanya ajione yuko age sawa na wewe... Mama angu ni wa kwenda mango garden jamani? sijawahi... Mama angu ni wa kukaa mpaka usiku wa manane kwenye wanja za starehe? Sijawahi.. Mama angu leo hii ni wa kumlisha maneno ya uongo na kweli akaonekana mbele ya binaadam ananikana mtoto wake wa kumzaa...?

Muna ulichomfanya mama angu Mungu ndo anajua na ipo siku isio na jina basi atakuadhirisha ila kaa ukitambua watoto wake wote hatupendi... So back to topic ya leo, umeona uendeleze ushenzi wako kwa kuanza kutunga uongo kwa watu wangu wa karibu... kama ulivyotangaza kwenye magroup yako kuwa unanipa mabwana...

Hivi Rose, mimi leo hii wewe unitaftie bwana kwakuwa wewe hutaki mabwana wa maana... Honey mimi sitafutiwagwi bwana... Mabwana wananitongoza wenyewe na mara nyingi nakuwa na mtu ninaempenda sio niliotafutiwa... Mimi sio mtoto mdogo...

Sasa naona umeanza na @junaithar kesho na kesho kutwa usiwasahau @directorjoan na @sweetlorah ... Afadhali hawa dada zangu naweza kuwapostia hata biashara zao na wakanilipa ... Niambie nini umefanya kwangu wewe.. Umenidhulumu

Tuesday, October 25, 2016

Mabadiliko yanayokuathiri wewe mwajiriwa na Ajira yako


Kwa Tanzania sasa hivi kupoteza kazi yako ni rahisi sana. Unaweza kwenda kazini leo ukakuta umefukuzwa.

Teknolojia inabadilisha kila kitu. Baada ya muda mfupi unaweza kukuta kazi yako inafanywa na mashine.

Kumbuka Sikwambii haya kukutia hofu ni Ukweli ili ujiandae Lolote laweza kutokea.

Mambo uliyokua huyajui:-

• Hakuna Tajiri alieajiriwa,matajiri wote wanamiliki biashara zao wenyewe. Usifikiri kuwa tajiri kwa kupitia kwenye ajira.

•  Huwezi kua tajiri kwa kutegemea mshahara wako anza sasa kufikiria na kufanya, buni mfumo utakaokutengenezea kipato wakati upo kwenye ajira kipato hicho kikizidi mshahara na fanya mpango uache kazi.

•  Kama hujui ni kwamba boss wako hana mpango wa kubadili maisha yako furaha yake yeye ni aone unamfanyia kazi kwa bidii. Ukiumwa leo ukabaki nyumbani miezi mitatu ukirudi kazini utakuta nafasi yako imeshachukuliwa.

•  Haijalishi una elimu kubwa kiasi gani au ndogo kiasi gani mwajiriwa ni mwajiriwa tu wote wana hatari moja/wote wanamfanyia kazi mtu, ukifukuzwa kazi leo maisha yako lazima yatayumba.

•  Kilio kimoja cha kila mwajiriwa ni mishahara haikutani. Unaweza kubadili hali hiyo leo kwa kua na mfumo wako unakutengenezea pesa nje ya ajira.

•  Usipoteze muda kuomba uongezewe mshahara au upande cheo waza kumiliki biashara yako mwenyewe.

•  Mshahara ukiongezeka ujue utatakiwa ufanye kazi nyingi zaidi/uzalishe Zaidi, ukipanda cheo ujue na majukumu yatakua mengi Zaidi. Pesa utakayoongezewa huwezi kuifurahia tena.

•  Kwenye mfumo wako mwenyewe ni kwamba kuna wakati utakua haupo lakini pesa zinaendelea kutengenezwa.

•  Kama unafarijiwa na mafao utakayopata uzeeni piga mahesabu ni kiasi gani utapokea na uone jinsi gani unapoteza muda.

•  Mafao unayoyasubiria baada ya miaka 40 ya ajira ungeweze kutengeneza mara 50 yake na kwa muendelezo yaani hiyo miaka 40 ya ajira ni miaka 5 tu inaweza kukufanya wewe uanze kuishi maisha ya kipato kinacholingana na mafao yako.

•  Ajira yako haikulindi bali inakufanya uwe mtumwa unauza muda na nguvu zako kila siku kipato ambacho siku zote hakitakaa kikutoshe.

•  Sikwambii haya ili uache kazi leo lah! Anza kujitengenezea mfumo leo ili undoke hapo bila maumivu wala hofu yeyote.

•  Zipo biashara nyingi za kuanza ukiwa kwenye ajira lakini changamoto kubwa ni kwamba zitakukosa wewe kwasababu upo kwenye ajira hivyo ukuaji wake utakua kwenye hatari kubwa sana.

•  Lakini zipo biashara ambazo unaweza kutenga ule muda wako wa ziada baada ya ajira ukawa unaikuza biashara hii na ikakuletea mafanikio makubwa sana.

Inawezekana wewe hujawahi kufikiria kua tajiri au kumiliki mali nyingi biashara zako na kadhalika lakini kujiajiri au kuwa na kipato cha ziada ni kitu cha muhimu kwa maana unakua hutegemei mshahara peke yake. Lolote linaweza kutokea kipindi hiki.

Kuwa makini na jitengezee njia za kukisaidia kabla mabaya hayajakufikia.

Mifumo ipo,

Tafakari, Chukua hatua
Huku ukimtanguliza Mwenyezi Mungu mbele.

VISA VYA WANAWAKE NA KUPONEA KUFA CHUPUCHUPU

NINGEKUFA KWA AJILI YA  MWANAMKE!!

Leo nimepita kisimani nikamkuta dada mmmoja akifua. ,Nikamuuliza eti dada unavijua visa vya wanawake??

Akajibu kaka niache, nikakomaa anijibu...
Badala ya kujbu akaanza kupiga mayowe, na kelele za kuomba msaada.. hadi wananchi wenye mapanga, mawe na mishale wakaanza kuja, dada huyo alivyoona wanakuja akajmwagia maji mwili mzima. Nikajua leo ndio mwisho wangu nikajuta sana kutaka kujua kila kitu..

Wananchi walivyofika, wakamuulza, kuna nini? Akawajibu, nilidumbukia kwenye kisima na huyu kaka ndie amensaidia!!
Wakanipongeza sana sana kisha wakaondoka...

Yule dada  akaniambia, hivyo ndivyo visa vya mwanamke anaweza kukuua au kukulinda! So muheshmu mwanamke hata kinafiki, usijfanye jeuri!!!

*KUOLEWA NI NDOTO KUU YA KILA MWANAMKE ALIYEKAMILIKA ILA KAMA UNA TABIA HIZI UTAZEEKEA NYUMBANI*


*1. Tamaa ya utajiri* fedha na mali nyingi pasipo kutambua kuwa vitu hutafutwa, hapa wengi hupoteza nyota zao kwa kukataa wengi wenye kipato cha kawaida na kujirahisisha kwa wenye nazo ambao kwa bahati mbaya wengi wao sio waoaji bali ni wahuni tu na watu wa anasa na kula bata mjin.

*2. Dharau,* maringo, kiburi na mashauzi yaani we kila mtu akikusogelea na kujaribu kuzungumza na wewe unaanza kumpandisha na kumshusha kisha una msonya. Wengi huishia kukupotezea wakijua either umewadharau au tayari una mtu wako ndio maana nyodo nyingi.

*3. Husali* hakika lazima wahuni watapata nafasi kwako na kukuchezea mpaka uchakae kama mtumba wa uvira. MWENYEZI MUNGU ndo  anaetoa BARAKA ukimuomba hakika atakuepushia kuingia midomon mwa dubu na fisi wanaokuwa wakikuvizia na kuja kama MALAIKA. Atakupa ufahamu wa kuwatambua na kuwashtukia mapema.

*4. Kuvaa nguo za ajabu ajabu kama changudoa*
. Sijui ni nani aliyewaambia kuwa mkivaa hivyo mnapendeza! Unakuta binti unavaa kama mcheza show za Casino yaani ukipita nguo yaonyesha kila kitu ukiinama ndio balaa kabisa yaani kimin kinafunuka kila kitu nje nje kwa style hiyo nani atakupeleka kwao?

*5. Kujipaka marangi ya ajabu ajabu usoni kama mwali wa kibembe*
au kizaramo kwanza mnatutisha tu.

*6. Kupenda kujirahisisha au kujipendekeza pendekeza kwa wanaume,*
yani ukiguswa kidogo tu twende.

*7. Kuwa na picha karibia 500 Facebook,* Twitter nk halafu picha zenyewe hazieleweki yani zimepigwa katika mavazi au mapozi ya ajabu ajabu, mara umebinua makalio, mara tumbo, mara mdomo,

*8. Kila unachofanya basi unakimbilia kupost mfano kwenye Facebook* na kadhalika
nyinginezo hata ukienda haja basi lazima upost.

*9. Ni mtu wa maneno maneno*
yani we kila unachokiona unaongea na kuropoka ropoka tu hauna break! mwanamke gani?

*10. Huna mawazo ya malengo* endelevu yani we kwenye kichwa chako kumejaa umbea tu sijui leo Wema Sepetu amefanya nini? Sijui Kim, Lupita amefanya vile na upuuzi mwingine.

*11 Mizinga.*
Yani siku ya pili tu baada ya kukutongoza unaanza " honey nataka galaxy" Htc" Huawei" mara baby nimeona nguo nzuri mara ooh baby yaani njaa inauma'' , utasindikiza harusi za wenzio hadi upigwe alama..

Waswahili husema, "Kama mzuri, Olewa"

Jihadhari na tabia hizi.
_Maneno makali ila ujumbe umefika.

Monday, October 24, 2016

Wanawake kuchunguzwa majeraha


Dar es Salaam. Wanawake na wasichana wasiopungua 250,  Oktoba 29 watafanyiwa uchunguzi wa majeraha ya viungo kutokana na ulemavu na ngozi.

Uchunguzi huo utafanywa na Taasisi ya Huduma za Afya ya Aga Khan, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la WomenforWomen kutoka Marekani.

Meneja Miradi wa Aga Khan, Nasreen Hassanali amesema jana kuwa watakaobainika kuathirika zaidi na ulemavu wa viungo na ngozi uliotokana na majanga ya moto na ajali watafanyiwa upasuaji bure kurekebisha sehemu hizo.

Alisema kambi ya uchunguzi itafanyika katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa saba mchana itakayoongozwa na daktari bingwa, Edwin Mrema.

HEKIMA YA LEO


*MAISHA YANA VITU 7,*

*1:- Furaha.*
*2:- Karaha.*
*3:- Misukosuko.*
*4:- Majonzi.*
*5:- Migogoro.*
*6:- Mikasa.*
*7:- Chuki.*

*Haya yote husababishwa na viumbe hai kama mimi na wewe, ili kuyashinda haya yakupasa uwe na mambo 4.*

*1:- Subira.*
*2:- Uelewa.*
*3:- Uvumilivu.*
*4:- Msamaha.*

*Lakini katika maisha yako pendelea sana kuwa na mambo 4.*

*1:- Msimamo.*
*2:- Mkweli.*
*3:- Ujasiri.*
*4:- Imani.*

*Ila epuka sana mambo 5.*

*1:- Udanganyifu.*
*2:- Uchoyo.*
*3:- Ubinafsi.*
*4:- Wizi.*
*5:- Kufitinisha.*

*Kumbuka kumjali anaekujali hata kama yupo mbali nawe.*
*Mpende anaekupenda hata kama hana kitu jali utu kuliko kitu.*
*Ibada ndo Nuru yako Duniani na Akhera.*

*Yaarabbi tupe Mwisho Mwemaa!!!*

Tuesday, October 18, 2016

BABA NIFUNDISHE KUHUSU WANAWAKE


"Nikufundishe nini mwanangu kuhusu wanawake? Baba yako nimezeeka ghafla nikiwa na ufahamu mdogo na mwanangu umeshakua kiasi cha kuhitaji elimu hii adhimu, nikupe neno gani?, labda hivi,

1.KUHUSU TAMAA ZAO. -Mwanamke yeyote anaweza kukutamani kimapenzi isipokuwa Mama yako.

2. KUHUSU HULKA ZAO.
-Wanawake wote huonesha upendo wao waziwazi isipokuwa wale waliotendwa kabla.

3.KUHUSU KUACHANA.
-Mwanaume kumuacha mwanamke anayempenda ni kama simba kuacha kula swala, Mwanamke kumuacha mwanaume ni rahisi kama swala kumkimbia Simba mzee.

4.KUHUSU TABIA.
-Jihadhari na maneno ya vijiweni kwamba wanawake wote wako sawa kitabia. No, lakini kumbuka hakuna Mwanamke asie Mwanamke.

5. KUHUSU MPENZI WA ZAMANI.
-Kujaribu kumsahau mwanamke uliyewahi kumpenda ni kama kumkumbuka mtu usiyemjua. Ni ngumu.

6. KUHUSU KUOA.
-Muhimu kuoa, na ni ngumu sana Kumjua mke mwema kabla ya kuoa, ni waigizaji wazuri sana. Kumbuka maneno ya Albert. " Muhimu kuoa, ukipata mke mwema utakuwa na furaha, ukipata mke mwovu utakuwa mwanafalsafa.

7. KUHUSU USALITI.
-Vizuri kujiandaa kisaikolojia kusalitiwa, la usipojiandaa ama waweza kuua mtu au hata kujiua. ukiua mtu maisha yako yatakosa furaha siku zote, ukijiua mwenyewe, hao waliokusaliti wanaweza kuishi kwa furaha zaidi ya ulivyokuwa hai.

8.KUHUSU PESA NA MAPENZI.
-Mapenzi bila pesa yanapatikana kwa wingi sana huko mbinguni, hapa duniani ni ngumu mno, lakini usihofu sana, kuna makubaliano bila pesa. Omba mungu.

9. KUHUSU UONGO.
-Wahenga walisema Ukweli unauma, Na mimi nakuambia "Uongo unaua"

10. KUHUSU KUWAJUA WANAWAKE.
-Ewe mwanangu, kutaka kumjua mwanamke unahitaji miaka mingi ya kuishi kuliko idadi ya nywele zao. Usihangaike na vitabu, makala, majarida, filamu, nyimbo na hotuba za wanaofundisha mandhari za wanawake. Kuna kanuni moja tu ya kupenda, " ili ubaki salama katika kupenda sharti ujipende kwanza".

...Basi mwanangu hayo ndio machache naweza kukuhusia, na wewe una nafasi ya kujifunza zaidi na kufundisha kwa ufanisi zaidi kuliko Mimi...
Umependa elimu gan hapo??

Thursday, October 13, 2016

MODELING INSPIRATION


Kila kinacho fanyika ndani ya maisha yetu ya kila siku kinaongozwa na nia,utayari,kujiamini,kujituma na kujisimamia"

Haiwezi kuwa rahisi mtu kutimiza ndoto zako katika maisha juu ya kile unacho kitazamia kama wewe mwenyewe haupo tayari kuona ndoto zako zikifanikiwa katika hilo :

Huyu ni model anayeishi South Africa .Ni model mwenye Albinism :

Hata siku moja hakutaka kuishi kwa kuikubali hali yake ya udhaifu wa ngozi,jamii inavyo mchukulia na jinsi hali nzima ya muonekano wake wa mwili ilivyo (Albino) ILA tangu akiwa na umri mdogo alijiandalia njia na mazingira mazuri ya kuiaminisha jamii kuwa anaweza na nimfano wa kuigwa :

Siku zote aliishi kwa kuamini yeye ni mshindi na nibora zaidi katika kila anacho kifanya kutetea ndoto zake za maisha kupitia modeling HAKURUHUSU hata siku moja mawazo na mitazamo ya watu wanao mzunguka viweze kumkatisha tamaa na kujihisi hana tena thamani katika dunia ya kuishi maisha ya ndoto zake:

Daima alitia nia na kujituma zaidi katika kuutafuta ushindi wa mawazo,uhuru,mafanikio na imani ya kile alicho kuwa anakitamania na kukiamini kwa muda mrefu kama sehemu ya maisha yake (modeling)............................... Wakati anaanza safari yake ya matumaini katika kupigania ndoto zake ndani ya modeling alianza na neno "Ipo siku" na alivyo zidi kusogea mbele zaidi akasema tena "Nimefika lakini bado si sehemu nayo taka kuwa"....................................... Furaha yake na lengo lake kubwa ilikuwa ni siku moja kutambulika na kuheshimika  zaidi Africa na dunia kwa ujumla kama South Africa's First International Male Model with Albinism na kweli mpaka sasa furaha yake katika ndoto hizo imesha onekana nakuwa sehemu ya mfano wa kuigwa :

Tulio wengi katika kuishi maisha ya kufanikiwa ndani ya ndoto zetu tulizo jiwekea huwa tunashindwa kufanikiwa na kuonekana wenye kukataa tamaa kwa sababu ya kutokuwa na msimamo wa mawazo,nia,kujiamini,utayari,kuthubutu na kujitokeza............................................... Unacho takiwa kujua ni kwamba maamuzi ya nguvu za kufanikiwa katika kile unacho kiamini kama sehemu ya maisha yako "vipo juu yako"

Shirikisho la walemavu limemvaa Waziri wa Afya


SHIRIKISHO la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) limeitaka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee kuwatambua watu wenye ulemavu kama kundi linalostahili kupata msamaha katika ulipiaji wa gharama za huduma za afya

Ummy Mwalimu Wazira wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee
Hatua hii inakuja ikiwa ni siku nne tu tangu Ummy Mwalimu,  Waziri wa wizara hiyo kuyataja makundi matatu yanayostahili kupata msamaha wa gharama za matibabu kuwa ni; watoto, wazee na wanawake wajawazito pekee.

Ummy Nderiananga, Mwenyekiti wa Shivyawata amewambia wanahabari leo jijini Dar es Salaam kuwa taarifa ya waziri Ummy Mwalimu kutolitaja kundi la walemavu kama sehemu ya makundi yanayosahili msamaha wa gharama za matibabu imeibua mjadala wenye hisia tofauti hasa kwa watu wenye ulemavu.

“Shivyawata inamtaka Waziri Ummy Mwalimu kuhakikisha kwamba waraka wa afya wa mwaka 2012, unawafikia watoa huduma za afya wa serikali kwani watu wenye ulemavu tunakabiliana na changamoto ya kutakiwa kuonyesha utambulisho maalumu kutoka serikali za mitaa.

Walemavu hatustahili kuhurumiwa bali kuzingatiwa kwa haki yetu ya msingi ya kupata huduma za afya bure kama makundi mengine,” amesema.

Nderiananga ameitaka Wizara ya Afya kufanya maboresho ya waraka wa afya wa mwaka 2012 ili huduma ya tiba bila malipo kwa walemavu isiishie kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati, bali pia katika hospitali za rufaa.

“Lakini pia Shivyawata tunaitaka Wizara ya Afya kutoa bima maalum za afya kwa watu wenye ulemavu ili kuepuka udhalilishaji na urasimu katika kupata huduma hizo katika vituo vya afya, zahanati na hospitali zote,” amesema Nderiananga.

Wednesday, October 12, 2016

CHEKA KIDOGO

*mama mwenye nyumba anajipodoa anashinda saloon kujipodoa lakini house girl hata mafuta usoni hapaki lakini akipita na khanga yake moja tuu nyumba inatetemeka���������������������������� huu mchezo hautaki mekapu*

SOMA HISTORIA YA CHE” GUEVARA MWANAMAPINDUZI HATARI DUNIANI,ALIYEONGOZA MAPINDUZI NCHINI CUBA

49 YEARS AFTER HIS ASSASSINATION:CELEBRATING LIFE & TIMES OF CHE GUEVARA

Jina lake halisi:Dr.ERNESTO RAFAEL GUEVARA de La Serna
Aliyefariki tarehe kama ya leo:9/10/1967

Mahali alipofia:La Higuera,Valle Grande-Bolivia.
Mzaliwa wa mji wa Rozario-Argentina,aliyepata masomo yake ya Udaktari katika chuo kikuu cha Bunos Airea(University of Bunos Aires)
Akiwa amezaliwa ktk familia yenye kipato cha kati,kwa leo tungemuita “mtoto wa kishua” CHE
Akiwa amebakiza mwaka mmoja kabla ya kumaliza masomo yake ya Udaktari,alitumia likizo kusafiri kwa pikipiki (Motorcycle) akiwa na rafikiye ALBERTO GRANADO na kutembea katika mataifa mbalimbali ya Amerika kusini ikiwemo Peru,Guatemala na akiwa katika,Safari alishuhudua Umasikini uliokithiri,Maradhi na unyonyaji wa jamii kutoka kwa makampuni ya kibwanyenye yaliyowekeza katika Amerika kusini.Akiwa Guatemala alishuhudia kupinduliwa kwa Rais Mzalendo,JACOB ALBERZ aliyechaguliwa na wananchi akiwa amelenga kurudisha Ardhi iliyokua imeporwa na Kampuni ya Kimarekani;AMERICAN FRUIT COMPANY.

Rais JACOB ALBERZ alipinduliwa kwa mpango wa CIA waliolenga kulinda maslahi ya Kampuni AMERICAN FRUIT COMPANY
Kwa mujibu wa yeye mwenyewe CHE GUEVARA katika Memoir yake,anasema alitamani baada ya kumaliza Masomo yake ya Udaktari ajikite hasa katika utafiti,awe mtafiti(Researcher)
Lakini kile alichokishuhudia GUATEMALA,PERU nk.kilitosha kubadili mawazo kuona kuna haja ya kuwa Mwananapinduzi kukomboa jamii kubwa aliyotopea ktk Umasikini na Unyonyaji
Baada ya kuhitimu masomo yake ya Udaktari aliondoka Argentina kuelekea Mexico alikokutana na RAUL CASTRO na FIDEL CASTRO wakiwa uhamishoni baada ya jaribio la kuvamia kambi ya jeshi ya Moncada na kumpindua Dikteta Fulgencio Batista kushindikana ikiwa ni mwaka 1957
Wakitumia Boat kwa jina “GRANMA” kutoka MEXICO walisafiri hadi CUBA walipoanza mapambano ya kumuondoa Dikteta Kibaraka wa marekani Fulgencio Batista,vita iliyodumu kwa miaka miwili mpaka mwaka mpya mwaka 1959 walipofanikiwa kuingia HAVANA wakitokea Milima ya Sierra Maestra,Santiago de CUBA. walikopigana vita ya msituni kwa miaka miwili kupitia vugu vugu la Julai 26(Julai 26 movement) lilioaisisiwa mwaka 1953 wakati wa jaribio la kuvamia na kupora silaha ktk kambi ya Jeshi ya Moncada kufeli.

Mwaka mpya 1959 yaani 1/1/1959 FIDEL,RAUL,CHE na CAMILO waliingia Havana na kuhitimisha mapinduzi,huku wakishangiliwa na maelfu ya wa CUBA waliojitokeza kuwalaki wapambanaji mahiri wakombozi wa CUBA huku Dikteta kibaraka Fulgencio Batista akikimbilia Marekani
Baada ya mapinduzi CHE alipewa majukumu makuu matatu:Waziri wa Viwanda,Mkuu wa Idara ya Ulinzi na Mkuu wa Benki kuu aliyesaini sarafu ya CUBA. “Peso” kwa jina lake “CHE”
Baada ya Mapinduzi FIDEL alimtuma CHE GUEVARA Katika mataifa mbali mbali kuimarisha Urafiki alikwenda Ulaya,Urusi,Asia na Afrika katika mataifa ya Algeria,Guinea,Misri nk.
Baada ya Safari hii aligundua bado kuna Mataifa mengi hayajapata Uhuru na Vita ya ukombozi inaendelea kuanzia Afrika,Asia na Amerika kusini pia.
Baada ya kukamilisha Ziara hii ndefu aliporejea HAVANA aliandika barua na kujiuzulu vyeo vyake vyote serikalini ikiwa ni pamoja na Uraia wa CUBA aliupata baada ya mapinduzi ya mwaja 1959.
Katika Barua ya kujiuzulu aliyomwandikia FIDEL alimweleza haoni sababu ya kuwa na vyeo serikalini wakati bado kuna watu wanateseka ktk mataifa mbalimbali,alimoumba FIDEL na serikali imtunzie Mkewe ALEIDA MARCH na Wanawe Ernesto,Aleida,Rafael maana inawezekana wanaweza wasimuone tena.Barua hii ilisomwa ba FIDEL ktk mkutano wa Hadhara jijini HAVANA waCUBA walilia na kusikitika juu ya maamuzi ya CHE
CHE alielekea ZAIRE(DRC) ya sasa akipitia Tanganyika(Tanzania) akivuka Ziwa Tanganyika na wapiganaji wake kadhaa aliotoka nao CUBA.Wakati huo LAURENT KABILA akiwa msituni anapigana kumuondoa Dikteta MOBUTU SE SEKO.CHE alikatishwa tamaa na udhaifu wa wapiganaji walioongozwa na Laurent Kabila walijikita kwenye Ulevi,ngono na Uporaji wa madini,CHE alirejea Tanganyika akikaa kwa muda na hatimaye kuelekea Bolivia ambapo wapiganaji walikua wakipigana na serikali Dhalimu.
Huku CIA wakimfuatilia wakimtumia kibaraka wao raia wa Cuba aliyekimbia marekani baada ya Mapinduzi FELIX RODRIGUEZ.ambaye alihibitisha uwepo wa CHE Bolivia
“CHE” alikamatwa na jeshi la Bolivia kwa maelekezo ya CIA akafungiwa katika nyumba moja iliyoko ktk eneo la Shule ktk kijiji cha LA HIGUERA-Mji wa Valle Grande baada ya mapigano makali na kupigwa risasi mguuni hivo kushindwa kukimbia hatimaye kukamatwa,ambapo FELIX RODRIGUEZ alituma telegraph Washington akajibiwa CHE GHEVARA auawe
Saa sita mchana tarehe 9/10/1967 kijana mdogo mwenye cheo cha Sajenti aitwaye:MARIO TERAN akiwa amelewa aliingia ktk Chumba alichokua amefungwa “CHE” na Bunduki
CHE GUEVARA alilomuona alimwambia “NAJUA UMEKUJA KUNIUA,NIPIGE RISASI WE MUOGA ILA UJUE UNAUA MWANAUME” English; “I KNOW YOU COME TO KILL ME,SHOOT COWARD BUT YOU ARE GOING TO KILL A MAN”
Habari za kuuawa CHE GUEVARA zilisambaa ulimwengu mzima kukawa na maombolezo na maandamano maeneo mbalimbali ulimwenguni kupinga Mauaji yake.Mwili wa CHE ulikatwa viganja kwa ajili ya CIA Kujiridhisha km ni CHE GUEVARA aliyeuawa kwa vipimo vya DNA.
CHE alizikwa katika kaburi la siri ambalo halikujulikana mpaka mwaka 2007 wataalamu(Archeologist) walipogundua kaburi lake huko Valle-Grande,Bolivia,Mabaki ya mwili wake yalipelekwa CUBA kwa Ndege maalum na kuhifadhiwa katika jengo la Makumbusho la CHE GUEVARA(CHE GUEVARA Museleom)-Jijini HAVANA
Mtoto pekee wa CHE GUEVARA ambaye yuko hai leo ni Dr.ALEIDA GUEVARA,Daktari bingwa wa watoto(Pediatrician) aliyeachwa na Baba akiwa na mwaka mmoja,ambaye serikali ya CUBA ilihudumia familia ya CHE baada ya kifo chake
Huyo ndo CHE GUEVARA kwa kifupi ambaye T-shirt zake zinavaliwa sana,Picha yake ni mashuhuri sana ktk stika za magari,na maeneo mbalimbali Ulimwenguni
Ceremos Como CHE,yaani “Tutakua kama CHE“ ni kauli mbiu ambayo watoto wadogo wa shule za msingi Nchini CUBA hufunzwa na kutumiwa km salam:CEREMOS COMO CHE
Long Live COMMANDANTE
Viva La Revolucion
HASTA LA VICTORIA SIEMPRE…!!! Until Victory Forever
Patria O Muerte,Vencermos ……… Homeland or Death,We shall Overcome
VIVA Commandante CHE GUEVARA

Monday, October 3, 2016

True star Rukia

This is #truestar Rukia, the oldest resident of #Kabangacentre. Like many older persons, she has special needs. Even more so because she was born with albinism. 

At 58 she has not been able to shine her light onto the world .

For #international #day of #olderpersons we want to enohasize that, PWAs, whether children or full-grown adults, have the right to be themselves and live in freedom in their communities or wherever they choose to be!

From one of albinism society foundation found at kigoma @kabangastars  - letthemshine #kabangastars #kabanga #kigoma #kasulu #kabangacenter #beautifulplace #beautifulpeople #pwa #albinismawareness #internationalolderpersonsday #ngo #socialprojects #takeaction #inmyskiniwin #happymonday

Tuesday, September 20, 2016

Fund for Daniel

@Regrann from @realjaype  -  @Regrann from @iamtjan -  Pls lets not forget to donate something for Daniel.. It's not a project! It's a cause that is personal to his family and myself and also everyone... Daniel is currently on a potential donor list in India and we can do more and do better guys ! ��  I understand the importance of giving so much cos I have known what it felt like to want something and not have it... You can fund Daniel here https://www.gofundme.com/29ume2ng  Or Donate to #GiveDanielAHeart FCMB - USUANLELE DANIEL OSAYANDE FCMB 3469556012  #GiveDanielAHeart Your Prayers and Donations Go a long way Dear Nigerian.  #TeamDaniel #Regrann - #regrann 

Tuesday, September 6, 2016

TANGAZA HAPA BUREEEE

Je umewahi kufikiri kabisa wapo vijana kwa ajili ya kusaidiana basi karibu katika tovuti hii.

Hipo kwa ajili ya vijana wote kujitangaza kwa kazi zao buree,pengine hata pasipo kujuwa mtu husika.

Umenielewa sasa wewe jitangaze popote kwani ndio muda wako.

KUTANA NA MALILA AU MALILERLOVEDEJO ANAE JIKUBALI KULIKO UNAVYO FIKIRI

Marafiki ndio chanzo pengine tukashindwa kuaminiana..

Unaweza ukawaamini kufanya nao kazi waka kudondosha..

Kutana na malila machim peter au @Malilerlovedejo kijana mwanaharakati na mfanyaji wa kazi za sanaa pia ni mwanamitindo.

Niliamini rafiki zangu kupitia walivyo kuwa navyo yani ujuzi kufanya nao kazi nao na waka mdondosha.

Alitaka blog yake tu itengenezwe iwe nzuri tu.. akahamua ampe dili rafiki yake bado still akuweza kumtimizia ndoto yake ikiwa ni rafiki wapili kumpatia iliaweze kusaidia pia kutangaza, vipaji vya vijana na rafiki zake.

Achana na izo tu kwa uchache hata biashara alizo fanya na marafiki zake na kuhamini pia walimdondosha..

Amebaki na ndoto na Harakati zake mwenyewe na hakiamini katika yeye mwenyewe. kuwatangaza bila gharama yeyote na kuwa na imani kwa vijana wenzake wanaweza.

Kijana huyu anasema anajiamini yeye tu.. katika kutengeneza mtazamo chanya kupitia mitandao ya kijamii na anaona matunda yake.

Huyo ndio malila machim au muhite Lovedejo.. "anasema kidogo kibaya ..kutokujua pia ni nyenzo ya mafanikio.na jikubali Mimi tu.

Friday, August 5, 2016

LISSU AFIKISHWA TENA MAHAKAMANI

Dar es Salaam. Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu amefikisha Mahakamani  ya Kisutu saa  8. 46  huku mahakamani hapo kukiwa na ulinzi mkali.

Ulinzi umeimarishwa katika mahakamani hapo muda mrefu wakati wakimsubiria Lissu akitokea katika kituo cha polisi kanda maalumu.

Polisi wapatao tisa baadhi ya wakiwa na silaha  wametanda katika eneo la mbele la mahakama hiyo.

HOMA YA MANJANO: WHO LAWAMANI


Uchunguzi wa shirika la habari la AP umebaini kwamba shirika la afya duniani WHO lilitekeleza makosa makubwa katika kukabiliana na mlipuko wa homa ya manjano Afrika ya Kati.

Uchunguzi huo unasema chanjo milioni moja zilizokuwa zikisafirishwa hadi Angola zilitoweka kutoka kwenye shehena ya chanjo milioni sita za homa hiyo ya manjano.

Baadhi ya chanjo zilipelekwa katika maeneo ambayo hayakuwa yameathiriwa na homa hiyo, huku zilizopelekwa katika maeneo yaliyoathiriwa, zikikosa sindano.

#BBC

Wednesday, August 3, 2016

WAFANYAKAZI WA CHINA WASHAMBULIWA KENYA:


Kundi moja la vijana waliojawa na ghadhabu na ambao walikuwa wamejihami na fimbo waliwavamia raia wa Uchina wanaofanya kazi ya ujenzi wa barabara ya kisasa ya Treni nchini Kenya.

Wafanyikazi 14 wa China walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo katika eneo la Narok, takriban kikomita 200 kusini magharibi mwa mji wa Nairobi.

Washambuliaji hao walidaiwa kulalamikia kampuni ya kujenga barabara na madaraja ya China kwa kutowapatia ajira za ujenzi wa reli hiyo.

Makumi ya maafisa wa polisi wamepelekwa katika eneo hilo huku mamlaka ikifanya mikutano ya dharura kwa lengo la kutuliza hali.

Kuna Takriban raia 4000 wa China wanaofanya kazi nchini Kenya hususan katika viwanda vya ujenzi pamoja na biashara za kuuza vifaa vya kielektroniki.

#BBC

Tuesday, August 2, 2016

Trump asema Hillary Clinton ni 'shetani'

Trump asema Hillary Clinton ni 'shetani'

Mgombea wa chama cha Republican nchini marekani Donald Trump amemtaja mshindani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton kuwa 'shetani'.

Akizungumza kwenye mkutano huko Pennsylvania bwana Trump alimshambulia Bernie Sanders kwa kumuachia nafasi Bi Clinton.
Tajiri huyo alisema kuwa Sanders alifanya makubaliano na 'shetani'.

Wanachama wa Democrat na Republican wememkosoa bwana Trump kutokana na matamshi yake kuhusu wazazi wa mwanajeshi M'marekani muislamu aliyeuawa vitani nchini Iraq.

WAZIRI MKUU AYAKATAA MADAWATI YA TFS


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekataa kupokea msaada wa madawati uliotolewa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) baada ya kubaini yametengenezwa chini ya kiwango. “Ofisa elimu njoo kagua haya madawati yaliyo mazuri nitayapokea na yaliyobaki yarudishwe karakana yakatengenezwe upya huu si wakati wa kupokea vitu vibovu,“ amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo wakati alipowasili katika kiwanja cha Mabau, Mtibwa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi ambapo alikabidhiwa madawati hayo na Meneja wa TFS.

Amesema anatambua dhamira ya TFS ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kumaliza tatizo la upungufu wa madawati lakini hawezi kupokea kupokea madawati yaliyotengenezwa chini ya kiwango.

AKATWA MIKONO KWA 'KUKOSA KUSHIKA MIMBA' KENYA:


Mwanamume mmoja nchini Kenya amedaiwa kumkata mikono yote miwili mkewe kwa kutumia kisu kikubwa kwa kushindwa kumzalia watoto,katika kile kinasemekana ni kisa kibaya zaidi cha ugomvi wa nyumbani.

Mikono ya Jackline Mwende kutoka kijiji cha Kathama ,Masii katika kaunti ya Machakos ilikatwa kutoka katika kifundo cha mkono na mumewe Stephen Ngila Thenge tarehe 24 mwezi Julai.

Pia ana majeraha katika kichwa chake na shingo kutokana na shambulio hilo.

Ndugu zake wanasema kuwa wanandoa hao walikuwa na matatizo na kwamba bi Mwende alitaka kumwacha mumewe,lakini akashauriwa kutofanya hivyo na kiongozi mmoja wa dini.

Mwende anasema kuwa kabla ya shambulio hilo walikuwa wakiishi mbalimbali na mumewe kwa takriban miezi mitatu kwa kosa la kutopata watoto. ''Sijui kwa nini aikuwa akinilaumu licha ya sisi sote kwenda hospitalini mwaka uliopita na kwamba daktari alisema kuwa ni yeye aliyekuwa na tatizo la kuzaa ambalo linaweza kurekebishwa''. Anasema kuwa mumewe ambaye ni mshonaji nguo katika mji wa Masii alikataa kufuatilia matibabu.

#BBC

Monday, August 1, 2016

MAANDAMANO: WATU 10 WAUAWA ETHIOPIA.

Makumi ya maelfu ya watu kutoka kabila la Amharic wameshiriki katika maandamano dhidi ya Serikali nchini Ethiopia katika mji wa kaskazini wa Gondar.

Waandamanaji hao wameitaka serikali kubadilisha uamuzi wake wa kuanzisha wilaya chini ya usimamizi wa kabila la Tigray.

Serikali ya Ethiopia inasema kuwa zaidi ya watu 10 wameuawa wakati wa makabiliano na polisi kuhusu eneo linalozozaniwa katika majuma ya hivi karibuni.

JIFUNZE WEWE MWANAMKE ULIYE SINGLE.

Tambua lengo lako kabla hujaingia kwenye ndoa.

Fanya biashara yoyote, tafuta shughuli ya kufanya.

Usimsubiri mwanaume ndio useme unaanza maisha.

Ongeza thamani ya maisha yako kwa kujenga maisha yako.

WALIMU MBARONI KWA KUNYWA POMBE SAA ZA KAZI

Sengerema. Baadhi ya walimu wa shule ya msingi Chifunfu katika Halmashauri ya Sengerema mkoani Mwanza wamekamatwa baada ya kukutwa wakinywa pombe saa za kazi.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Chifunfu, Lucas Mashinji amesema walimu hao walikutwa baa Julai 29 saa 3.15 asubuhi, baada ya raia wema kutoa taarifa kwa diwani wa eneo hilo, Robert Madaha.

Mashinji amesema walimu hao wanashikiliwa ofisi ya kata wakisubuiri taratibu nyingine kufanyika.

Diwani Madaha alisema taarifa za walimu hao alizipata kutoka kwa wananchi kuwa walimu hao wapo baa hivyo alitoa maagizo wakamatwe.

Sunday, July 31, 2016

MWANAMKE MKONGWE ZIMBABWE

Mwanamke mkongwe nchini Zimbabwe, wakati wa maandamano nje ya ukumbi wa baraza la jiji la Bulawayo.

Walikuwa wanaonesha kwamba hawana vyakula vya kutosha kutokana na kudorora kwa uchumi.

Picha/AFP, Getty #bbcswahili #Zimbabwe #mwanamke:

DRC:UPINZANI WAMTAKA KABILA AACHIE MADARAKA.

Makumi ya maelfu ya wafuasi wa upinzani wamekusanyika mjini Kinshasa, Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, kupinga uwezekano kuwa uchaguzi wa rais huenda ukaahirishwa.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanywa Novemba, lakini tume ya uchaguzi, imesema inaweza kuchukua miezi 16, kurekibisha orodha za wapigaji kura.Upinzani unaona kuna jaribio la kuahirisha uchaguzi, ili kumruhusu rais Joseph Kabila abakie madarakani.

Kufuatana na katiba ya nchi hiyo kubwa ya Afrika , Rais Kabila anatakiwa kuondoka madarakani mwaka huu, baada ya kutumika kwa mihula miwili.Hata hivyo mahakama ya kikatiba nchini humo yameamua abakie madarakani, hadi uchaguzi utapofanywa.

#BBC:

BREAKING NEWS.....

Mhe Lembeli amerudi chama kubwa CCM hivi mchana wa leo katika mkutano mkubwa wa Mhe Mwenyekiti wa CCM na rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli... Huko mjini Kahama. Anasema haoni sababu ya kwenda na "..safari ya uhakika isiyo na uhakika... kule hamna kitu."


MAFURIKO YAUA ZAIDI YA WATU 100 INDIA NA NEPAL:

Mafuriko mashariki mwa India na nchini Nepal yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 100 na kuwaathiri mamilioni ya wengine.

Mito iliyojaa maji imesababisha vijiji kufurika na kuwalazimu maelfu ya watu kuhama makwao.

Katika majimbo ya India ya Assam na Bihar, makundi ya uokoaji yanatumia mashua kuwafikia watu ambao wametafuta hifadhi katika makao ya muda kwenye sehemu zilizoinuka.

#BBC 

Saturday, July 30, 2016

MBOWE AITWA POLISI, LOWASSA AZUIWA DAR:

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Rais John Magufuli na Chadema kutoa misimamo tofauti kuhusu kupigwa marufuku kwa mikutano ya kisiasa, Jeshi la Polisi limemuita Freeman Mbowe kwa mahojiano, huku hafla ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili ambayo Edward Lowassa angekuwa mgeni rasmi ikizuiwa.

Katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji naye ameendelea kusisitiza msimamo wa chama chake wa kuitisha mikutano nchi nzima Septemba Mosi, kauli aliyoitoa saa chache baada ya Rais Magufuli kusisitiza msimamo wa kuzuia maandamano na mikutano ya kisiasa isipokuwa kwa wale walioshinda kwenye udiwani na ubunge ambao watatakiwa kufanya hivyo kwenye maeneo yao tu. #mwananchi 

Monday, July 25, 2016

WABUNGE WA CHADEMA KIKAANGONI Arusha.

Jeshi la polisi mkoani Arusha, limewaita kwa mahojiano, mbunge wa Karatu,Wilbroad Qambalo, mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso na Mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu,Jubilate Mnyenye kutokana na kupuuza agizo la kutofanya mikutano ya hadhara katika jimbo hilo. Mwingine ambaye ametakiwa kwenda kuripoti polisi ni Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu, Lazaro Bajuta.

Wakizungumza jana baada ya kukabidhiwa barua za wito wa polisi, Qambalo na Paresso walisema wamestuka kutakiwa kuripoti ofisi ofisi ya Mkuu wa upelelezi mkoa wa Arusha jumatano.

Parreso alisema,walipokea barua jana saa sita mchana na kutakiwa kuripoti kwa RCO, saa nane lakini wakampigia na kumweleza wana ratiba nyingine tayari waende jumatano na akakubali.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkombo alipotakiwa kuelezea agizo hilo alisema yupo likizo.

WAZIRI MKUU KUHAMIA DODOMA SEPTEMBA Dodoma. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo asubuhi wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma. 

“Jana nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma ifikapo Septemba,” amesema Majaliwa na kushangiliwa na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma waliohudhuria maadhimisho hayo. 

Amesema tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, kazi nyingi zimefanyika na wananchi wameziona na kwamba sasa hivi kazi iliyobakia ni utekelezaji wa ahadi alizotoa Rais John Magufuli.

 “Wananchi kazi mmeziona na sasa tunaenda kwenye utekelezaji. Ninatoa agizo kuwa mawaziri na manaibu wote wahame mara moja kutoka Dar es Salaam na kuja Dodoma. 

Wana ofisi ndogo Dodoma na kwa kuwa wamekuwa wakiishi wakati wote wa Bunge, wahamie mara moja. Mimi nahamia Septemba na utekelezaji wake nitausimamia kwa juhudi zote,” alisisitiza. 

Amewataka wakazi wa Dodoma watumie fursa hiyo kutunza amani ya nchi na kudumisha umoja uliopo na pia akataka watumie fursa hiyo kujenga nyumba za kuishi za kutosha, nyumba za kulala wageni na hoteli za kitalii ili watu watumishi na wageni wanapokuja wasipate taabu mahali pa kuishi.

Sunday, July 24, 2016

KIJANA KIONGOZI KWA MIFANO

HUYU NDIO YULE ANAEVAA SUTI NA KUANGAIKIA AU KUELIMISHA KUHUSU ALIBINISIMU@suleimanmagoma

Moja ya sehemu zinazo nipa mkate wa kila siku. Am very grateful to this place and i love my job.. Karibuni HASHTAG SQUARE  tunauza juice ya miwa iliyoandaliwa katika mazingira yanayozingatia Usafi. Utapata  Juice ya Miwa pamoja na bites mbalimbali.
Tunapatikana stendi ya Makumbusho lango la kutokea Magari mkabala na mti wa mbuyu. Karibuni sana mniunge mkono.

Cku mojamoja mtu mzima  nasimamia  mpango mzima mwenyewe.Kuwa na maisha bora c jambo rahisi ni lazima Upige kazi kwelikweli na uwe mbunifu kila kukicha  na kumuomba Allah.. wengi waliofanikiwa wametumia njia hizo. Nawashangaa sana baadhi ya watanzania wenzangu ambao hawataki kufanya kazi  wanaamini eti Kiungo cha Mtu mwenye Albinism kina leta Utajiri. Tuwapuuze watu wenye fikra na mitazamo hiyo na Tuwape Elimu ya kutosha ili waelewe kuwa hamna shotcut katika maisha inabid wajitume katika kufanya kazi zilizo halali. #albinismawarenessfoundation

KARIBUNI sana HASHTAG SQUARE

MHAMIAJI 'KUTOKA SYRIA' AJILIPUA UJERUMANI:

Wakuu katika maeneo ya Kusini mwa Ujerumani, wamesema kuwa mtu mmoja amejilipua ndani ya baa na kuwajeruhi watu wengine 12, watatu kati yao vibaya sana.

Maafisa wa serikali wanasema mshukiwa ni raia wa Syria ambaye alikuwa ameshindwa kupata hifadhi nchini Ujerumani mwaka jana.Mlipuko huo ulitokea katika mji wa Ansbach karibu na tamasha moja la muziki ambalo ni maarufu sana katika eneo hilo.
Zaidi ya watu elfu mbili wameondolewa kutoka katika tamasha hilo, ambalo baadaye lilisitishwa.
Baadhi ya maeneo ya mji huo wa Ansbach, yamezingirwa na walinda usalama.Ni shambulio la tatu huko Bavaria, katika kipindi cha wiki moja.Ijumaa, watu tisa walifariki shambulio la ufyatuaji risasi mjini Munich na siku chache awali, kijana aliwashambulia watu kwa kisu na shoka kwenye treni.
#BBC

DK. SHEIN AFUATA NYAYO ZA JPM:

Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, amefuta uteuzi wa Naibu Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Hafidh Ussi Haji huku akimteua Khadija Shamte Mzee, kuchukua nafasi hiyo.

Pia, taarifa ya Ikulu inaonyesha Dk Shein, amemteua Amour Hamil Bakari kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar kuchukua nafasi ya Abdi Khamis Faki ambaye anastaafu kwa mujibu wa sheria.

Vilevile, Dk Shein amemteua Umi Aley kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Magazeti ya Serikali; Said Bakar Jecha na Sebtuu Mohammed Nassor wameteuliwa kuwa Makamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, wakati Ali Saleh Mwinyikai ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Zanzibar.

Wengine walioteuliwa ni Maryam Hamdan kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni, wakati Maryam Abdulla Yussuf ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani Zanzibar na Profesa Ali Seif Mshimba, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Zanzibar. Uteuzi huo unaanza Julai 25.

TCU YAFUNGIA VYUO VINGINE KUDAHILI.

BAADA ya wiki jana kutangaza orodha ya vyuo ambavyo havitaruhusiwa kudahili Wanafunzi Kwa Mwaka wa Masomo 2016/17, leo Tume hiyo imetoa orodha nyingine ya vyuo ambavyo vimefungiwa kufanya udahili kutokana na sababu mbalimbali. Vyuo vilivyozuiwa kudahili ni pamoja na;

1. Katavi University of Agriculture - Kozi zote.

2. Ekernforde Tanga University - Kozi zote.

3. Hubert Kairuki Memorial University - Kozi ya udaktari.

4. Muslim University of Morogoro - Kozi ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma.

5. St. Joseph University In Tanzania (St.Mark's University College) - Kozi zote.

6. United African University of Tanzania - Kozi zote.

7. Tanzania International University - Kozi zote.

8. Kampala International University, Dar es Salaam College - Kozi ya Sayansi ya Kompyuta.

9. St. Joseph University College of Management and Commerce - Kozi zote.

10. Tumaini University, Dar es Salaam College - Kozi ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma.

12. Stefano Moshi Memorial University College - Kozi zote.

13. Teofilo Kisanji University, Tabora campus - Kozi zote.

14. University of Arusha, Musoma campus - Kozi zote.

15. Mount Meru University, Mwanza campus - Kozi zote.

16. University of Mbeya - Kozi zote.

17. Mzumbe University, Mwanza campus - Kozi zote.

18. Stella Maris Mtwara University College - Kozi zote.

19. ArchBishop James University College - Kozi zote.

20. Mwalimu Julius K. Nyerere University of Science and Technology - Kozi zote.

21. Josiah Kibira University College - Kozi zote.

22. College of Business Education, Mwanza campus - Kozi zote za shahada na shahada na Shahada ya Uzamili.

Kwa taarifa zaidi tembelea
http://www.tcu.go.tz

Watoto wenye ualbino wapewa mafuta maalum ya kulinda ngozi

Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Gilbert Simya na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga Robert Mageni waliosimama nyuma wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa chama cha albino wilaya ya Mbinga, baada ya kukabidhi msaada wa mafuta yenye thamani ya shilingi laki 8 yaliyotolewa na chama cha walemavu wilayani humo kwa ufadhili wa hospitali ya KCMC ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma Robert Mageni,akiteta jambo na mtoto mwenye ualbino ambaye hakufahamika jina lake mara moja wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mafuta maalum ya kuzuia magonjwa kwa watu wenye ulamavu wa ngozi yaliyotolewa na chama cha albino wilaya ya Mbinga.

Sista Judith Mwageni wa shirika la mtakatifu Wiliam jimbo la Mbinga akiwatambulisha watoto wenye ualbino wanaolelewa na kanisa katoriki jimbo la Mbinga wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa mafuta maalum ya kuzuia magonjwa ya ngozi yaliyotolewa na chama cha walemavu wilaya ya Mbinga.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga Robert Magenj akizungumza jana katika hafla ya kukabidhi mafuta maalum kwa watu wenye ualbino yaliyotolewa na chama cha walemavu wilaya ya Mbinga kwa ufadhili wa hospitali ya KCMC ya Moshi,katikati ni katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Gilbert Simya.

Katibu tawala wa wilaya ya Mbinga Gilbert Simya akitoa mafuta maalum ya kuzuia magonjwa kwa watu wenye ualbino jana wakati wa kukabidhi msaada wa mafuta wenye thamani ya shlingi laki 8 yaliyotolewa na chama cha walemavu wilayani humo.Picha na Muhidin Amri.

Saturday, July 16, 2016

TUCHEKE KIDOGO

*Zuberi* alimpa ujauzito mwanafunzi
akashtakiwa.
Kumbe Zuberi ana bibi
yake mtaalamu wa yale mambo yao
ya Sumbawanga, akampachika Zuberi
jinsia ya kike alipofika mahakamani
kuhojiwa Zuberi akasema sijampa ujauzito kwani mimi nina jinsia ya kike.
Kwa kuthibitisha Zuberi akajifunua
nguo basi akashinda kesi, kufika
nyumbani Zuberi akawakuta watu
wamejaa wanalia, akauliza kulikoni?
Akaambiwa bibi yako amefariki.
Zuberi akawa *zubeda*������������������

Friday, July 8, 2016

AFARIKI DUNIA KWA MASHINE YA KUSAGIA KOKOTO

Mfanyakazi mmoja ametumbukia kwenye mtambo wa kusagia kokoto kwa bahati mbaya. Nandio ukawa mwisho wake wa kuishi. Imetokea huku mbeya

Thursday, May 26, 2016

TAS MOROGORO INATOA PONGEZI KWA WAZAZI, WENYE WATOTO WALIO NA HALI YA ALIBINO.

Kuhusu utunzaji bora wa mtoto mwenye ualbino nimuhimu sana mfano mzuri ni dadaetu Hawa Hassan tulimpatia Elimu ya ufahamu kusu malezi bora ya mtoto wake Wema.

Na leo mtoto huyu amekuwa kivutio kwakila mtu jinsi muonekano wa mtoto Wema anavyo onekana.

Hongera sana mama Wema na wazazi wengine kwa kutusikiliza ushauri wetu ambao umepelekea Wema Kuwa na afya bora ya ngozi.

Alisema mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualibino mkoa wa morogoro Bw.Hassan mikazi.

KANSA KWA WATU WENYE UALIBINO INAWEZEKANA

Kama wazazi na walezi watapatiwa Elimu ya kumtunza mtoto mwenye ualbino tatizo la saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino litapungua sana.

Nimuda muafaka sasa kwa wadau na serikali kutoa kuwapatia sunscreen lotion kwakila mtu mwenye ualbino ili kupunguza saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino hususan watoto.

Mkoa wa Morogoro unakadiriwa kuwa na watu wenye ualbino zaidi ya 15,000 wengiwao wanaishi vijijini na hawapatiwi vifaa tiba wala vifaakinga kama sunscreen lotion hali inayopelekea kuasirika na tatizo la saratani ya ngozi

BREAKING NEWZZ...

DIAMOND ÑA ALIKIBA WAPIGANA STUDIO

Wakiwa ndani ya studio ya Burn Records inayomilikiwa na 'chalii' Shedy Clever usiku msanii Diamond na hasimu wake mkubwa katika gemu la Bongofleva Alikiba..kulitokea mabishano makali kati ya wasanii hao hali iliyomnyima moyo wa subira Diamond na kujikuta akimrushia ngumi msanii mwenzake Alikiba...

Muda mchache uliopita inasemekana kwamba producer Shedy Clever aliwapigià simu wasanii hao akiwataka waende studio kwake kwa ajili ya kuwasikilizisha 'beats' alizoziandaa kwa ajili yao...
Katika hali ambayo kila mmoja hakutegemea kumkuta mwenzake studio hapo ilimpa wakati mgumu producer shedy baada ya wasanii hao kujikuta wakivutiwa na beat moja na kila mmoja alihitaji kulichukua kwa ajili ya kulitumia...
Wakati wakiendelea kugombea beat hilo walijikuta wakirushiana ngumi hali iliyopelekea kuvunjika kwa Computer ya studio humo...
Baada ya ugomvi kuwa mkali Shedy clever aliamua kupiga simu polisi na baada ya polisi kufika waliwakamata wasanii hao na kuwapeleka kituoni kwa mahojiano zaidi.....
                *     *      *
*JAMANIEEE NIKO FIELD NAJIFUNZA KUANDIKA HABARI ZA UDAKU......"*

Tuesday, May 24, 2016

ULIKUWA UJUI CHUKUWA HIYO

  ����������������������������������������
1. Kama upo SINGLE na umekazana kusema "SIAMINI MTU KATIKA MAPENZI" kumbuka rafiki zako wanaoa na kuolewa kila siku. Acha mawazo hasi omba Mungu akujalie mwenza wa maisha ambae unaendana nae.

2. Kama upo ndani ya ndoa na umekazana kusema "NAICHUKIA HII NDOA" huoni wanandoa wengine ambao wanasheherekea jubilei ya miaka 20 ya ndoa zao?  Omba Mungu aiponye ndoa yako.

3. Kama umekazana kusema "NAMWACHA MUME WANGU, KWANI ANANISALITI" tafadhali hebu nenda mjini pita maeneo ya Kona Bar, Kimboka na maeneo kama hayo uone wanawake malaya wenye uchu ambao wanamsubiri kwa hamu mumeo wamchune vizuri ambao kwao hawajali haya ku share mwanaume. Omba Mungu aitengeneze ndoa yako.

4. Usikazane kusema "NAICHUKIA KAZI YANGU" angalia maelfu ya vijana ambao hawana ajira wanazunguka kila siku na mabahasha maofisini! Vipi unataka kujiunga nao? Kuwa na shukrani!

5. Umekazana kusema unapachukia unapoishi, tafadhali sana nenda kawatembelee watoto wa mitaani uone mazingira magumu wanayoishi! Mshukuru Mungu walau unalala hata kwenye godoro.

6. Wengine husema "NIMECHOKA NA HAYA MAISHA" sawa nenda mahospitalini na uone watu wanavyopigania maisha yao, nenda mochwari na utizame na uniambie unafikiri nini! Cha Mihimu ni kushukuru Mungu

HEBU NISIKILIZE KWA MAKINI..... Kutambua thamani ya miaka minne au mitatu, muulize mhitimu wa chuo kikuu

Kutambua thamani ya mwaka mmoja, muulize mwanafunzi aliyefeli mtihani wake wa mwisho, kutambua umuhimu wa miezi tisa muulize mama aliejifungua mtoto aliye njiti!

Kutambua thamani ya wiki moja muulize mhariri wa gazeti linalotoka kila wiki.

Kutambua thamani ya dakika moja muulize abiria aliyechelewa safari ya ndege, basi au treni.

Na kutambua thamani ya sekunde muulize mtu yeyote aliyenusurika katika ajali!

Furahia kila dakika ambayo mwenyezi Mungu amekupa kuendelea kuvuta pumzi yake! Acha kulalamika maisha ni jinsi wewe unavyoishi!

Kama upo hai mpaka leo shukuru kwa kusema "ASANTE MUNGU"

Share it with your friend

Monday, May 23, 2016

KASHIFA YA CHINA NA NYAMA ZA BINADAMU WAFU

CHINA YAKANA KUUZA NYAMA YA BINADAMU AFRIKA
Wizara ya maswala ya kigeni nchini China imekana ripoti kwamba kampuni za chakula nchini humo zinaweka nyama ya binaadamu na kuuza barani Afrika kama nyama ya ng'ombe.

Chombo cha habari nchini humo Xhinua kimesema kuwa jarida moja nchini Zambia lilimnukuu kimakosa mwanamke mmoja ambaye hakutajwa anayeishi China.

Alisema kuwa kampuni za China zilikuwa zikichukua miili ya wafu kuitia katika viungo na kuiweka katika mikebe.

Msemaji wa China Hong Lei amesema kuwa ripoti hizo hazina uwajibikaji.

Balozi wa China nchini Zambia,Yang Youming ,amesema kuwa ripoti hizo zililenga kuharibu uhusiano mzuri kati ya mataifa hayo mawili. ''Leo jarida moja linasambaza uvumi ,likidai China inatumia nyama ya binaadamu ambayo uihifadhi katika mikebe na kuiuza Afrika. ''Hii ni dhulma ya makusudi ambayo haiwezi kukubalika kabisa kwetu sisi''.
#BBC

WANAWAKE NI TATIZO HILI

WANAUME TUSHIRIKI KATIKA SALA HII YA KUWAOMBEA WANAWAKE ...

1. Atakua na simu yake mpo nyumbani dakika hiyo anakwambia umbip hajui kaiweka wapi.
- Tuhurumie Baba

2. Ana Nguo zimejaa makabati mawili lakini hajui avae nini ukimwambia mtoke!
- Baba, ni magumu kwetu mambo haya.

3. Anakasirika ukikosa kumtumia text ya good night lakini yeye akikosa wewe inabidi uwe muelewa!
- Tuwaeleweje, Baba?

4. Ana viatu zaidi ya pea 50 lakini hana viatu vya kuvaa vya kwenda ibadani.
- Mungu uwasamehe

5. Akianza kuvaa saa moja atamaliza saa tano muda wote inabidi umsubiri tu.
- Si kupenda kwao Baba ila nasi yanatushinda Bwana

6. Akienda saloon anakaa kuanzia asubuhi mpaka jioni na huna budi kumsubiri na usilalamike.
- Mungu wetu, tupe moyo wa kuyahimili haya

7. Ana mafuta tofauti ya kujipaka mikono, shingo, kisogo, miguu, mpaka kisigino! Hata Mdomoni
- Ee Mungu ni Wewe uyajuaye mateso tuyapitiayo Baba

8. Mnaachana asubuhi akiwa na furaha, na ukirudi jioni amenuna hataki hata kukusalamia na ukiuliza tu balaa.
- Tupe uvumilivu ee Bwana!

9. Anajaribu ku match nguo na hereni na akiona hazifanani abadili nguo sababu tu ya hereni.
- Teremka uwashike mikono yao baba..

10. Mkitembea barabarani inabidi ukae upande wa barabara eti wewe ni mwanaume ukigongwa na gari haina noma.
- Eeh baba tuepushe na Hiki kikombe ulisema hawa ni wasaidizi wetu lakini tumekuja kuwa wafanyakazi wao.

Amen!!!!!!!!!!

JIFUNZE EWE MWANAMKE


1. Usikimbilie kuhama na kuondoka nyumbani kwa wazazi wako kabla hujajipanga vizuri.

2. Usimsubiri mwanaume ndio uanze maisha, unaweza ukaishi maisha yako mwenyewe na ukaweka msingi mzuri utakaokusaidia huko baadae.

3. Kaa mbali na marafiki waovu, jifunze kuheshimu kila mtu kuwa na busara na vaa mavazi ya heshima.

4. Usimchekee chekee kila mwanaume, kwa maana wengine sio waoaji ni chui waliojivika ngozi ya kondoo! Ni bora ukaendelea kuabki single kuliko uje kuolewa na mtu ambaye atakufanya ujute maisha yako yote hapa duniani. Omba Mungu akupe busara na ustahimilivu.

5. Jijengee tabia ya kula kwa afya, siku zote jitahidi ule milo yote mitatu acha kula biscuit na soda, usipendelee chips na mishkaki na vyakula vya aina hiyo. Fanya mazoezi mepesi kuuweka mwili wako uendelee kuwa mzuri wa kuvutia. Wewe ni tunu kwa mume wako mtarajiwa au uliyenae.

6. Vaa kwa heshima, watu watakujaji kulingana na jinsi tu ulovyovaa hata maongezi yao yataegemea kutokana na uvaaji wako.

7. Usitumie SEX kama njia ya kujihakikishia Mapenzi. Kufanya mapenzi sio tiketi ya kupendwa. Ata SEX na wewe na atakuacha kwenye mataa ya ubungo junction.

8. Usiolewe nae kwa vile ana pesa za kutosha na ni tajiri kwa sababu karibuni tu na wewe utakua moja ya mali anazomiliki.

8. Jiongezee thamani, get a career! Usiwe mpumbavu kufikiri mwanaume ndio atasuluhisha matatizo yako yote. Jibidiishe kwa kazi zako binafsi hakuna raha juu ya kuwa na maamuzi ya kutumia kile kipato ulichokipata kwa jasho lako.

10. Wewe ni wa muhimu mno, una thamani kubwa sana! Jipende jiheshimu, jijali. Usijali umetendwa na wangapi katika mahusiano! Usikate tamaa jiweke vizuri. Ishi maisha yako. Hayo unayopitia ni funzo tu ktk maisha.

Above all, Remember this, Charm is deceitful, and beauty is vain: but a woman that fears the LORD, she shall be respected.

MUNGU AWABARIKI WANAWAKE WOTE ULIMWENGUNI, ABARIKI KAZI ZA MIKONO YENU NA SIO KAZI ZA MAUNGO YENU. NINYI NI WA THAMANI MNO.

Sunday, May 22, 2016

KIONGOZI WA TALIBAN AUAWA PAKISTAN

Kamanda mmoja mkuu nchini Afghanistan amethibitisha kuwa kiongozi mkuu wa wapiganaji wa kundi la Taliban, Mullah Akhtar Mansour, ameuwawa.
Mullah Abdul Rauf, ambaye majuzi alipatana tena na Mansour, baada ya kukosana aliponyimwa nafasi ya kuliongoza kundi hilo la wapiganaji, ameliambia shirika la Associated Press kuwa, Mansour aliuwawa siku ya Ijumaa kwa shambulio lililotekelezwa na Marekani mpakani mwa Afghanistan na Pakistan.
Inasemekana kuwa Rais Barack Obama aliidhinisha shambulio hilo mapema.
Serikali ya Afghan na Pakistani, zinasema kuwa hazikufahamishwa kuhusiana na shambulio hilo. #Regrann

ZIFUATAZO NI AINA SABA  ZA BUSU NA MAANA ZAKE

Butterfly kiss;

Hapa unambusu mwenza wako ukiwa kwenye zero distance, fungua kope zako polepole huku ukigusanisha kwenye shavu lake. Busu hili hutoa mtekenyo wenye kusisimua kwenye shavu.

Eskimo kiss

Huku mpo distance zero na mpenzi wako sugua pua yako kwenye pua yake kama sekunde 10 hivi, raha sana.

Finger kiss

Wakati mmelala wote na mpenzi wako, chukua kidole kimoja cha mkono wake na kibusu kwa kukinyonya.

French kiss

Hili ni busu linalohusisha ulimi wengine huita “soul kiss” kwa sababu uhai na nafsi hupita kwenda kwa mwingine kupitia kupumua kwa kinywa kupitia ulimi “wet”, aina hili la busu huhusisha maeneo yote ya mdomo na husisimua maeneo yote ya mwili.

Fruit kiss

Chukua kipande cha tunda (hasa fruit juice kipande cha nanasi, embe au zabibu) ng’ata nusu na yeye nusu na kunyang’anyana hadi zinavunjika na juice kuteremka midomoni kimahaba zaidi.

Tiger kiss

Kama tiger huku akiwa hajui ukiwa mgongoni mshike na kumbusu kwa kung’ata shingo (angalia usije muumiza mimi simo nazungumzia kung’ata kimahaba).

Earlobe Kiss

Polepole ingiza ulimi kwenye masikio na kuyanyonya, usifanye kwa kusababisha sauti sana kwani masikio ni sensitive sana kwa sauti.

Sikitiko La Mahaba Linashinda Msiba!

Hujaumia Subiri Usimuliwe!

Moyo Unapouma Kwa Sababu Ya Mapenzi Hakuna Kitu Cha Kupoza. Unaweza Kunywa Pombe Na Usilewe, Ukabugia Dawa Za Usingizi Na Usilale.
Kifua Kinajaa Na Kwa Sababu Inaathiri Mfumo Wa Upumuaji Na Mapafu Nayo Huingia Katika Maumivu.
Sikitiko La Mahaba Ni Hatari, Likikufika Utapungua Uzito Kwa Kasi Bila Maelezo Ya Ziada.

Chakula Hakiwezi Kupita Na Macho Yanaweza Kujaa Machozi Ilhali Unatamani Kujizuia. Binadamu Tumetofautiana, Wapo Wanaotamani Kupendwa Lakini Wengine Wanawacheza Shere Wanaowapenda.
Dawa Kuu Ni Kujihadhari Na Watu Wasio Na Mapenzi Ya Dhati.

Kuwaepuka Kadiri Inavyowezekana.

Ni Mzuri Na Anakuvutia Lakini Heri Umuone Kwa Mbali Kwa Sababu Ukimjaza Moyoni Atakusumbua.
Atakutoa Machozi Katika Eneo Ambalo Ulihitaji Kufurahi.
Maumivu Yako Hata Yajali Kwa Sababu Hana Hisia Na Wewe.

Atakusaliti Bila Woga Kwa Maana Hana Hofu Yoyote Juu Yako.
Itakuwa Ngumu Kumuacha, Vilevile Utaona Uamuzi Wowote Wa Kutengana Naye Ni Mateso Makubwa Kwamba Heri Uumie Ukiwa Naye Kuliko Kuachana.

Usijidanganye Ndugu Yangu, Wewe Ni Binadamu Uliyekamilika, Kwa Hiyo Usitarajie Mtu Wa Pili Au Wa Tatu Anaweza Kusikia Kile Kinachokuuma Moyoni.

Mateso Yaliyopo Ndani Yako Unayajua Mwenyewe, Kwa Hiyo Unatakiwa Kuwa Wa Kwanza Kujihurumia Na Kuchukua Uamuzi Wa Kujiokoa Na Mateso.

Kuna Kitu Kimoja Ambacho Unatakiwa Kukifahamu; Binadamu Ni Wa Ajabu Sana, Watayajua Yako Ya Siri Na Kile Ambacho Mwenzi Wako Anakifanya Pembeni, Lakini Hawakwambii Badala Yake Wataketi Pembeni Kuzungumza. “Aah Yule Wa Ajabu, Anadhani Kapata Mpenzi Kumbe Kapatikana!”

Wengine Utakaa Nao Meza Moja Kushauriana Mambo Mbalimbali, Lakini Anayekwambia Umvumilie Mwenzi Wako Licha Ya Vitimbi Anavyokufanyia, Ndiyo Huyo Huyo Akikaa Pembeni Na Watu Anawaambia Kwa Mtindo Wa Kukucheka Kwamba Unamng’ang’ania Mpenzi Bomu.

Lingine Ni Kuwa Unapokuwa Na Mpenzi Ambaye Hakuheshimu, Thamani Yako Katika Jamii Inashuka.
Kukuheshimu Si Mpaka Akutukane, Bali Vitendo Vyake. Kutoka Na Wapenzi Wengine, Kujenga Mazoea Na Watu Wa Jinsia Nyingine Kiasi Kwamba Mpaka Anahusishwa Kwamba Ni Wapenzi Wake.

Mathalan, Mpenzi Wako Anakuwa Na Urafiki Na Watu Mpaka Anafikiriwa Anatembea Nao.
Hii Ni Tabia Mbaya Na Haikubaliki, Ingawa Wapo Wazuri Wa Kutetea. Watasema, Sisi Ni Washkaji Ila Fahamu Mapenzi Yenu Yanazikutanisha Familia Mbili. Una Ndugu, Marafiki, Wazazi.

Inakuaje Mpenzi Wako Anahisiwa Anatoka Na Mwanamke Mwingine Na Taarifa Zinafika Mpaka Kwa Wazazi Wako? Watajua Mkwe Wao Ni Kicheche Na Hilo Litakugharimu Kwa Kiasi Kikubwa.

Unatakiwa Kulinda Thamani, Heshima Na Utu Wako, Kwa Hiyo Achana Na Mtu Asiyejua Maana!
Unaweza Kuona Leo Inakuuma Kwa Sababu Unaepukana Na Mtu Ambaye Unampenda Lakini Hiyo Ni Nafuu Kwako Kesho.
Amini Kwamba Mwisho Wa Mateso Hayo Ya Moyo Ni Furaha Kubwa, Mwisho Utajiuliza:

Ni Kipi Kilichokuwa Kinakufanya Uumie Kwa Muda Wote? Upo Huru Sasa!
Mapenzi Maana Yake Utulivu Wa Moyo, Yaani Wewe Na Mtu Wako Spesho Muogelee Katika Dimbwi Maalum, Ninyi Wote Mkiwa Na Amani.

Mkishirikiana Katika Hali Zote. Inakuwa Hakuna Anayewaza La Kwake Peke Yake Isipokuwa Kwa Ajili Yenu.
Ukilia Anakuwa Wa Kwanza Kukubembeleza, Anapogundua Amekuudhi Ni Mwepesi Kukuomba Msamaha.
Anasoma Mabadiliko Yako Na Kukuuliza Kile Kinachokusumbua.
Anaficha Siri Zako, Anazungumza Lugha Tamu Na Hisia Zake Zote Zipo Kwako. Kwa Wengine Haoni Hatamani.

USITHUBUTU KULAZIMISHA PENZI

Yamewafika Wengi Na Wameumia, Kwa Hiyo Ni Vizuri Kuwa Makini.
Utauguza Donda La Moyo Lisiloweza Kutibika, Utakonda Wenzako Watakucheka, Atakugeuza Punda Afanye Anachokitaka.
Ni Kazi Bure Kumpenda Mtu Asiyekupenda.
Pamoja Na Maumivu Unayoweza Kuyapata Lakini Kuna Vitu Hivi Lazima Vikukute Kwa Huyo Mwenzi Wako Wa Kulazimisha.

ATAKUTESA KWA UBINAFSI WAKE

Hana Mapenzi Ya Kweli Na Wewe, Kwa Hiyo Si Kila Wakati Atakufikiria.
Kama Hamjawa Kwenye Ndoa Itakusumbua Kwa Sababu Ni Ngumu Kufikiria Kwa Ajili Yenu, Isipokuwa Atawaza Kwa Matilaba Yake. Kama Kuoana, Utalazimisha Wewe Lakini Yeye Hatokuwa Na Habari.

Mkiwa Kwenye Ndoa, Hatojisikia Fahari Kutoka Na Wewe Atalazimisha Maisha Ya Kila Mmoja Kuwa Huru Kufanya Mambo Yake.
Nguo Atanunua Za Kwake Na Hata Siku Moja Hutoona Amekununulia. Wewe Utafanya Mengi Kwa Ajili Yake Lakini Yeye Atabaki Na Ubinafsi Wake.
Atakutesa, Pasha Moto Ubongo!

AKIONA WENGINE ATAHISI NI WAZURI ZAIDI YAKO!

Mtu Huishi Kwa Fikra Zake, Kwa Hiyo Kwa Sababu Hakupendi Kwa Moyo Wake Wote Inakuwa Ngumu Kukukubali, Hivyo Anapokutana Na Watu Wengine Barabarani Atadhani Ni Wazuri Kuliko Wewe. Atababaika Hata Mbele Yako.

Unahitaji Heshima Ya Kiwango Bora Na Kwa Kawaida Mpenzi Wako Anapaswa Kukuona Wewe Ni Mtu Namba Moja.
Kama Hakupi Nafasi Hiyo Maana Yake Anapenda Nusunusu Au Hapendi Kabisa.
Usikaribishe Mateso, Fikiria Kesho, Chukua Uamuzi Leo.

HASIFU MUONEKANO WAKO, ANA LAKE KICHWANI!
Hujiulizi, Kila Siku Anakuona Na Hakusifii! Ni Wazi Kuwa Hata Kama Wewe Ni Mzuri Kiasi Gani, Unavaa Na Kupendeza Kwa Namna Bora Kabisa Lakini Mwenzi Wako Hawezi Kukupa Pongezi Kwa Sababu Ana Lake Kichwani.

Ukiona Hilo Ujue Kwamba Yupo Mtu Ambaye Anamsifu Kwa Sababu Ndiye Anayemkubali, Na Wewe Utasifiwa Na Wengine.
Inauma Mwenzi Wako Kukuacha Nyumbani Na Kwenda Kumwaga Sifa Pembeni, Wakati Na Wewe Unazihitaji.
Una Thamani Kubwa, Pigania Utulivu Wa Moyo Wako!.......